Pular para o conteúdo
Publicidade

Hesabu 13:27,28,30-33

SRUV Swahili Revised Union Version

27 Kut 3:8;13:5;33:3;Kum 1:25Wakamwambia wakasema, Tulifika nchi ile uliyotutuma, kwa hakika, ni nchi yenye wingi wa maziwa na asali, uthibitisho, haya ndiyo matunda yake. 28 Kum 1:28;9:1,2Lakini watu wanaokaa katika nchi ile ni wenye nguvu, na miji yao ina maboma, nayo ni makubwa sana; na pamoja na hayo tuliwaona wana wa Anaki huko. 30 Yos 14:7;Zab 60:12;118:10;Isa 11:10;Rum 8:31;Flp 4:13;Ebr 11:33,34Kalebu akawatuliza watu mbele ya Musa, akasema, Na tupande mara moja tukaimiliki; maana twaweza kushinda bila shaka. 31 Bali wale watu waliopanda pamoja naye wakasema, Hatuwezi kupanda tupigane na watu hawa; kwa maana wana nguvu kuliko sisi. 32 Mt 23:13;Amo 2:9Wakawaletea wana wa Israeli habari mbaya ya ile nchi waliyoipeleleza, wakasema, Ile nchi tuliyopita kati yake ili kuipeleleza, ni nchi inayowala wakazi wake; na watu wote tuliowaona ndani yake ni watu wakubwa mno. 33 Mwa 6:4;1 Sam 17:4-7;Isa 40:22Kisha, huko tuliwaona Wanefili, wana wa Anaki, waliotoka kwa hao Wanefili; tukajiona nafsi zetu kuwa kama mapanzi; nao ndivyo walivyotuona sisi.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    27 Wakampa Musa taarifa hii: "Tuliingia katika nchi uliyotutuma, nayo inatiririka maziwa na asali! Hili hapa tunda lake. 28 Lakini watu wanaoishi huko ni wenye nguvu, na miji yao ina ngome na ni mikubwa sana. Huko tuliona hata wazao wa Anaki.

    30 Kisha Kalebu akawanyamazisha watu mbele ya Musa na kusema, "Imetupasa kupanda na kuimiliki nchi, kwa maana hakika tunaweza kufanya hivyo."

    31 Lakini watu waliokuwa wamepanda pamoja naye wakasema, "Hatuwezi kuwashambulia wale watu; wana nguvu kuliko sisi." 32 Wakaeneza taarifa mbaya miongoni mwa Waisraeli kuhusu nchi waliyoipeleleza. Wakasema, "Nchi tuliyoipeleleza hula watu wanaoishi ndani yake. Watu wote tuliowaona huko ni majitu. 33 Tuliwaona Wanefili huko (wazao wa Anaki wanatokana na Wanefili). Tulijiona kama panzi machoni petu wenyewe, nao ndivyo walivyotuona."

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    27 Wakampa Mose taarifa hii: "Tuliingia katika nchi uliyotutuma, nayo inatiririka maziwa na asali! Hili hapa tunda lake. 28 Lakini watu wanaoishi huko ni wenye nguvu, na miji yao ina ngome na ni mikubwa sana. Huko tuliona hata wazao wa Anaki.

    30 Kisha Kalebu akawanyamazisha watu mbele ya Mose na kusema, "Imetupasa kupanda na kuimiliki nchi, kwa maana hakika tunaweza kufanya hivyo."

    31 Lakini watu waliokuwa wamepanda pamoja naye wakasema, "Hatuwezi kuwashambulia wale watu; wana nguvu kutuliko sisi." 32 Wakaeneza taarifa mbaya miongoni mwa Waisraeli kuhusu nchi waliyoipeleleza. Wakasema, "Nchi tuliyoipeleleza hula watu waishio ndani yake. Watu wote tuliowaona huko ni majitu. 33 Tuliwaona Wanefili huko (wazao wa Anaki wanatokana na Wanefili.) Tulijiona kama panzi machoni petu wenyewe, nao ndivyo walivyotuona."

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.