Watu wanaasi
1 Usiku ule watu wote wa jumuiya walipaza sauti zao na kulia kwa sauti kuu. 2 Waisraeli wote wakanung’unika dhidi ya Musa na Haruni, na kusanyiko lote wakawaambia, "Laiti tungekuwa tumefia humo nchi ya Misri! Au humu kwenye hili jangwa! 3 Kwa nini Mwenyezi Mungu anatuleta katika nchi hii ili tufe kwa upanga? Wake zetu na watoto wetu watachukuliwa kama nyara. Je, isingekuwa bora kwetu kurudi Misri?"
9 Ila tu msimwasi Mwenyezi Mungu. Wala msiwaogope watu wa nchi hiyo, kwa sababu tutawameza. Ulinzi wao umeondoka, lakini Mwenyezi Mungu yupo pamoja nasi. Msiwaogope."
33 Watoto wenu watakuwa wachungaji wa mifugo hapa kwa miaka arobaini, wakiteseka kwa ajili ya kukosa uaminifu kwenu, hadi mwili wa mtu wenu wa mwisho ulale katika jangwa hili. 34 Kwa miaka arobaini, mwaka mmoja kwa kila siku katika zile siku arobaini mlizoipeleleza nchi, mtateseka kwa ajili ya dhambi zenu, na kujua jinsi ilivyo vibaya kunifanya mimi kuwa adui yenu.’