Watu wanaasi
1 Mkutano wote wakapaza sauti zao wakalia; watu wakatoka machozi usiku ule. 2 Zab 106:25;Kum 28:68Kisha wana wa Israeli wote wakamnung’unikia Musa na Haruni; mkutano wote wakawaambia, Ingekuwa heri kama tungalikufa katika nchi ya Misri, au, ingekuwa heri kama tungalikufa katika jangwa hili. 3 Mbona BWANA anatuleta mpaka nchi hii ili tuanguke kwa upanga? Wake zetu na watoto wetu watakuwa mateka; je! Si afadhali turudi Misri? 9 Ebr 3:16;Kum 9:7,23,24;Kum 20:3;Hes 24:8;Mwa 48:21;Kut 33:16;Kum 20:1;2 Nya 15:2;Isa 41:10Lakini msimwasi BWANA, wala msiwaogope wale wenyeji wa nchi, maana wao ni chakula kwetu; kinga iliyokuwa juu yao imeondolewa, naye BWANA yuko pamoja nasi; msiwaogope.
33 Mdo 7:36;Zab 107:40;Kum 2:14Kisha watoto wenu watakuwa wachungaji jangwani muda wa miaka arubaini nao watauchukua mzigo wa uasherati wenu, hadi maiti zenu zitakapoangamia jangwani. 34 Hes 13:25;Zab 95:10;Eze 4:6;1 Fal 8:56;Zab 77:8;Ebr 4:1Kwa jumla ya hizo siku mlizoipeleleza ile nchi, yaani, siku arubaini kila siku kuhesabiwa mwaka, mtayachukua maovu yenu, ndiyo miaka arubaini, nanyi mtakujua kuchukizwa kwangu.