Agano la Yonathani na Daudi
1 Mwa 44:30;2 Sam 18:33;Kol 2:2;Kum 13:6;1 Sam 19:2;20:17;2 Sam 1:26;Mit 18:24;Yn 15:17-19;1 Yoh 3:12-14Ikawa Daudi alipokwisha kusema na Sauli, roho ya Yonathani, ikaambatana na roho ya Daudi, Yonathani akampenda kama roho yake mwenyewe. 2 1 Sam 8:11;14:52;17:15Sauli akamtwaa siku ile, wala hakumwacha arudi tena nyumbani kwa baba yake. 3 Nao Yonathani na Daudi wakaahidiana, kwa kuwa alimpenda kama roho yake mwenyewe.