Pular para o conteúdo
Publicidade

2 Mambo ya Nyakati 7:12-15

SRUV Swahili Revised Union Version

Bwana amtokea Sulemani mara ya pili

12 Mwa 12:7;Kum 12:5;Zab 78:68,69;132:13,14BWANA akamtokea Sulemani usiku, akamwambia, Nimesikia uliyoyaomba, na mahali hapa nimejichagulia kuwa nyumba ya dhabihu. 13 2 Nya 6:26Nikizifunga mbingu isiwepo mvua, tena nikiamuru nzige kula nchi, au nikiwatumia watu wangu tauni; 14 Yak 4:10;2 Nya 6:27ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekeza, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao. 15 2 Nya 6:40Sasa macho yangu yatafumbuka, na masikio yangu yatasikiliza maombi ya watu waombao mahali hapa.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    12 Mwenyezi Mungu akamtokea Sulemani usiku na kumwambia:

    "Nimesikia maombi yako nami nimechagua mahali hapa kwa ajili yangu mwenyewe kuwa Hekalu kwa ajili ya dhabihu.

    13 "Nitakapofunga mbingu ili isiwepo mvua, au nikiamuru nzige kula mazao ya nchi au nikituma tauni miongoni mwa watu wangu, 14 ikiwa watu wangu, wanaoitwa kwa Jina langu, watajinyenyekeza na kuomba na kuutafuta uso wangu, na kuacha njia zao mbaya, basi nitasikia toka mbinguni na kuwasamehe dhambi yao, na nitaiponya nchi yao. 15 Sasa macho yangu yatafumbuka na masikio yangu yatasikiliza kwa makini maombi yanayoombwa mahali hapa.

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    12 Bwana akamtokea Solomoni usiku na kumwambia:

    "Nimesikia maombi yako nami nimechagua mahali hapa kwa ajili yangu mwenyewe kuwa Hekalu kwa ajili ya dhabihu.

    13 "Wakati nitakapofunga mbingu ili isiwepo mvua, au nikiamuru nzige kula mazao ya nchi au nikituma tauni miongoni mwa watu wangu, 14 kama watu wangu, wanaoitwa kwa Jina langu, watajinyenyekesha na kuomba na kuutafuta uso wangu na kuacha njia zao mbaya, basi nitasikia toka mbinguni na kuwasamehe dhambi yao na nitaiponya nchi yao. 15 Sasa macho yangu yatafumbuka na masikio yangu yatasikiliza kwa makini maombi yaombwayo mahali hapa.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.