Pular para o conteúdo
Publicidade

2 Reis 6

Muujiza wa shoka

1 1 Sam 10:12;2 Fal 2:3;4:1,38;9:1Kisha, wana wa manabii wakamwambia Elisha, Angalia basi, mahali tukaapo mbele yako ni padogo kwetu. 2 Basi twende mpaka Yordani, twakuomba, tutwae huko kila mtu mti mmoja, ili tujifanyie huko mahali pa kukaa. Akajibu, Haya! Nendeni. 3 Mmoja wao akasema, Uwe radhi, basi nakusihi, uende pamoja na watumishi wako. Akajibu, Nitakwenda. 4 Basi, akaenda pamoja nao. Nao walipofika Yordani, wakakata miti. 5 Lakini mmojawapo alipokuwa katika kukata boriti, chuma cha shoka kikaanguka majini; akalia, akasema, Ole wangu! Bwana wangu, kwani kiliazimiwa kile. 6 Kut 15:25;2 Fal 2:21;4:41Mtu wa Mungu akasema, Kilianguka wapi? Akamwonesha mahali. Akakata kijiti, akakitupa pale pale, chuma kikaelea. 7 Akasema, Kiokote. Basi akanyosha mkono, akakitwaa.

Veja também