Mto wa maji ya uzima
1 Eze 47:1;Zek 14:8Kisha akanionesha mto wa maji ya uzima, wenye kung’aa kama bilauri, ukitoka katika kiti cha enzi cha Mungu, na cha Mwana-kondoo, 2 Mwa 2:9;Eze 47:12;Ufu 21:21katikati ya njia yake kuu. Na upande huu na huu kando ya ule mto, ulikuwapo mti wa uzima, uzaao matunda, aina kumi na mbili, wenye kutoa matunda yake kila mwezi; na majani ya mti huo ni ya kuwaponya mataifa. 3 Zek 14:11Wala hapatakuwa na laana yoyote tena. Na kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana-kondoo kitakuwamo ndani yake. Na watumishi wake watamtumikia; 4 Mt 5:8;Ufu 3:12nao watamwona uso wake, na jina lake litakuwa katika vipaji vya nyuso zao. 5 Isa 60:19;Dan 7:18,27;Ufu 21:25Wala hapatakuwa na usiku tena; wala hawana haja ya taa wala ya nuru ya jua; kwa kuwa Bwana Mungu huwatia nuru, nao watatawala hata milele na milele.