Maelezo ya wasifu
1 Zab 45:13 Binti wa kimalkia, jinsi ulivyo mzuri
Hatua zako katika mitarawanda.
Mapaja yako ya mviringo ni kama johari,
Kazi ya mikono ya fundi stadi;
2 Kitovu chako ni kama bakuli la mviringo,
Na isikose divai iliyochanganyika;
Tumbo lako ni mfano wa chungu ya ngano,
Iliyozungukwa na ugo wa nyinyoro;
3 Wim 4:5 Matiti yako mawili ni kama wanapaa wawili,
Ambao ni mapacha ya paa;
4 Shingo yako ni kama huo mnara wa pembe;
Macho yako kama viziwa vya Heshboni,
Karibu na mlango wa Beth-rabi;
Pua yako ni kama mnara wa Lebanoni,
Unaoelekea Dameski;
5 Kichwa chako juu yako ni kama Karmeli,
Na nywele za kichwa chako kama urujuani,
Mfalme amenaswa na mashungi yake.
6 Jinsi yalivyo mazuri, yalivyo matamu,
Mapenzi katikati ya anasa!
7 Kimo chako kimefanana na mtende,
Na matiti yako na vichala.
8 Nilisema, Nitapanda huo mtende,
Na kuyashika makuti yake.
Matiti yako na yawe kama vichala vya mzabibu,
Na harufu ya pumzi yako kama mapera;
9 Na kinywa chako kama divai iliyo bora,
Kwa mpendwa wangu inashuka taratibu,
Ikitiririka midomoni mwao walalao.
10 Wim 2:16;Gal 2:20;Zab 45:11 Mimi ni wake mpendwa wangu,
Na shauku yake ni juu yangu.
11 Njoo, mpendwa wangu, twende mashambani,
Tufanye maskani katika vijiji.7:11 Au, penye maua ya mhina.
12 Wim 6:11;4:16;Zab 63:3-8;73:25 Twende mapema hadi mashamba ya mizabibu,
Tuone kama mzabibu umechanua,
Na maua yake yamefunuka;
Kama mikomamanga imetoa maua;
Huko nitakupa upendo wangu.
13 Mwa 30:14;Wim 5:1;Mt 13:52;Yn 15:8 Mitunguja hutoa harufu yake;
Juu ya milango yetu yako matunda mazuri,
Mapya na ya kale, ya kila namna,
Niliyokuwekea, mpendwa wangu.