16 Kut 23:2-8;Yn 7:24;Law 24:22Nikawaagiza wakati ule waamuzi wenu, nikawaambia, Sikilizeni ninyi maneno kati ya ndugu zenu, mkaamue kwa haki kati ya mtu na nduguye, na mgeni aliye pamoja naye. 17 1 Sam 16:7;Mit 24:23;Yak 2:1;Mit 28:21;29:4,25;2 Nya 19:6;Kut 18:22,26Msitazame nafsi za watu katika hukumu; muwasikize wadogo na wakubwa sawasawa; msiche uso wa mtu yeyote; kwa kuwa hukumu ni ya Mungu; na lile neno liwashindalo mniletee mimi, nami nitalisikiza.
Publicidade