Pular para o conteúdo
Publicidade

Kumbukumbu la Torati 10:1-5

SRUV Swahili Revised Union Version

Jozi ya pili ya mbao

1 Kut 34:1,2;25:10Wakati ule BWANA akaniambia, Chonga mbao mbili za mawe mfano wa zile za kwanza, kisha uje kwangu huku mlimani, ukajifanyie na sanduku la mti. 2 Nami nitaandika juu ya hizo mbao maneno hayo yaliyokuwa juu ya mbao za kwanza, ulizozivunja, nawe uzitie ndani ya hilo sanduku. 3 Kut 25:5;37:1Basi nikafanya sanduku la mti wa mshita, nikachonga mbao mbili za mawe mfano wa zile za kwanza, nikakwea mle mlimani, na zile mbao mbili mkononi mwangu. 4 Kut 34:28;Yer 31:33;Kut 20:1;19:17;Kum 9:10;18:16Naye akaandika juu ya mbao mfano wa maandiko ya kwanza, zile amri kumi,10:4 au maneno kumi. alizowaambia BWANA huko mlimani kutoka kati ya moto siku ya mkutano; BWANA akanipa. 5 Kut 34:29;40:20;1 Fal 8:9Basi nikageuka nikashuka kutoka mlimani, nikazitia mbao ndani ya sanduku nililofanya; nazo zimo humo kama alivyoniamuru BWANA.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    1 Wakati ule Mwenyezi Mungu aliniambia, "Chonga vibao viwili vya mawe kama vile vya kwanza uje kwangu juu mlimani. Pia utengeneze Sanduku la mbao. 2 Nitaandika juu ya vibao maneno yaliyokuwa katika vile vibao vya kwanza, ambavyo ulivivunja. Kisha utaviweka ndani ya Sanduku."

    3 Hivyo nikatengeneza Sanduku kwa mti wa mshita, nikachonga pia vibao vya mawe kama vile vya kwanza, kisha nikakwea mlimani nikiwa na vile vibao viwili mikononi mwangu. 4 Mwenyezi Mungu akaandika juu ya hivi vibao kile alichokuwa amekiandika kabla, Amri Kumi alizokuwa amewatangazia huko mlimani, kutoka kati ya moto siku ile ya kusanyiko. Mwenyezi Mungu akanikabidhi. 5 Kisha nikashuka kutoka mlimani na kuweka vibao ndani ya Sanduku nililokuwa nimelitengeneza, kama Mwenyezi Mungu alivyoniagiza, navyo viko huko sasa.

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    1 Wakati ule Bwana aliniambia, "Chonga vibao viwili vya mawe kama vile vya kwanza uje kwangu juu mlimani. Pia utengeneze Sanduku la mbao. 2 Nitaandika juu ya vibao maneno yaliyokuwa katika vile vibao vya kwanza, ambavyo ulivivunja. Kisha utaviweka ndani ya Sanduku."

    3 Hivyo nikatengeneza Sanduku kwa mti wa mshita, nikachonga pia vibao vya mawe kama vile vya kwanza, kisha nikakwea mlimani nikiwa na vibao viwili mikononi mwangu. 4 Bwana akaandika juu ya hivi vibao kile alichokuwa amekiandika kabla, Amri Kumi alizokuwa amewatangazia juu mlimani, kutoka kwenye moto siku ile ya kusanyiko. Bwana akanikabidhi. 5 Kisha nikashuka kutoka mlimani na kuweka vibao ndani ya Sanduku nililokuwa nimelitengeneza, kama Bwana alivyoniagiza, navyo viko huko sasa.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.