Pular para o conteúdo
Publicidade

Kumbukumbu la Torati 6

4 Mk 12:29;Isa 9:6;Yn 1:1;10:30;17:3;1 Kor 8:4;Efe 4:6;Flp 2:5,6Sikiliza, Ee Israeli; BWANA, Mungu wetu, BWANA ndiye mmoja6:4 Au Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja; au Bwana Mungu wetu ni mmoja; au Bwana ni Mungu wetu, Bwana ni mmoja.5 Mt 22:37;Mk 12:30-32;Lk 10:27;Kum 30:6;1 Yoh 5:3Nawe mpende BWANA, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote. 6 Kum 11:18-20;Isa 51:7Na maneno haya ninayokuamuru leo, yatakuwa katika moyo wako; 7 Efe 6:4nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyasema uishipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo. 8 Mit 6:21;Kut 13:9;Mit 3:3;7:3Yafunge yawe dalili juu ya mkono wako, nayo yatakuwa kama utepe katikati ya macho yako. 9 Kum 11:20;Isa 50:8;57:8Tena yaandike juu ya miimo ya nyumba yako, na juu ya malango yako.

Veja também