Pular para o conteúdo
Publicidade

Kutoka 12

24 Nanyi mtalitunza jambo hili kuwa ni amri kwako na kwa wanao milele. 25 Itakuwa hapo mtakapoifikia hiyo nchi, BWANA atakayowapa, kama alivyoahidi, ndipo mtakapoushika utumishi huu. 26 Kut 13:8,14;Kum 32:7;Yos 4:6;Zab 78:6Kisha itakuwa, hapo watoto wenu watakapowauliza, Ni nini maana yake utumishi huu kwenu? 27 Ndipo mtawaambia, Ni dhabihu ya Pasaka ya BWANA, kwa kuwa alipita juu ya nyumba za wana wa Israeli huko Misri, hapo alipowapiga Wamisri, akaziokoa nyumba zetu. Hao watu wakainamisha vichwa na kusujudia.

Veja também