2 Kut 15:24;Zab 106:25;1 Kor 10:10Na mkutano mzima wa wana wa Israeli ukawanung’unikia Musa na Haruni, huko barani; 3 Hes 11:4wana wa Israeli wakawaambia, Laiti tungalikufa kwa mkono wa BWANA katika nchi ya Misri, hapo tulipoketi karibu na zile sufuria za nyama, tulipokula vyakula hata kushiba; kwani mmetutoa huko na kututia katika bara hii, ili kutuua kwa njaa kusanyiko hili lote.