4 Kum 32:11;Isa 63:9;Ufu 12:14Mmeona jinsi nilivyowatendea Wamisri, na jinsi nilivyowachukua ninyi juu ya mbawa za tai, nikawaleta ninyi kwangu mimi. 5 Kum 4:20;7:6;10:14;14:2;26:18;32:8;1 Fal 8:53;Zab 50:12;135:4;Tit 2:14;1 Kor 10:26Sasa basi ikiwa mtaitii sauti yangu kweli kweli, na kulishika agano langu, hapo ndipo mtakapokuwa tunu kwangu kuliko makabila yote ya watu; maana dunia yote pia ni mali yangu, 6 Ufu 1:6;5:10;20:6;1 Pet 2:5,9;Law 20:24;Kum 7:6;Isa 62:12;1 The 5:27nanyi mtakuwa kwangu ufalme wa makuhani, na taifa takatifu. Hayo ndiyo maneno utakayowaambia wana wa Israeli.
Kutoka 19:4-6
Em outras traduções
- ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas
4 ‘Ninyi wenyewe mmeona nililofanya huko Misri, jinsi nilivyowabeba kwenye mabawa ya tai na kuwaleta kwangu. 5 Sasa, mkinitii kikamilifu na kutunza agano langu, basi ninyi mtakuwa hazina yangu ya pekee miongoni mwa mataifa yote. Ijapokuwa dunia yote ni mali yangu, 6 ninyi mtakuwa kwangu ufalme wa makuhani na taifa takatifu.’ Haya ndio maneno utakayosema kwa Waisraeli."
- ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli
4 ‘Ninyi wenyewe mmeona nililofanya huko Misri, jinsi nilivyowabeba kwenye mbawa za tai na kuwaleta kwangu. 5 Sasa kama mkinitii kikamilifu na kutunza Agano langu, basi ninyi mtakuwa mali yangu ya thamani kubwa miongoni mwa mataifa yote. Ijapokuwa dunia yote ni mali yangu, 6 ninyi mtakuwa kwangu ufalme wa makuhani na taifa takatifu.’ Haya ndiyo maneno utakayosema kwa wana wa Israeli."
Direitos das traduções citadas
Estes versículos te tocaram? Ore agora!
+581 estão orando agora.
Junte-se à corrente de oração.