Kuzaliwa na ujana wa Musa
1 Kut 6:20;Hes 26:59;1 Nya 23:13,14Mtu mmoja wa nyumba ya Lawi akaenda akaoa binti mmoja wa Lawi. 2 Mdo 7:20;Ebr 11:23Yule mwanamke akachukua mimba akazaa mwana, na alipoona ya kuwa ni mtoto mzuri akamficha miezi mitatu. 3 Na alipokuwa hawezi kumficha tena, akamtengenezea kikapu cha mafunjo akakitaliza kwa sifa na lami, akamtia mtoto ndani yake, akakiweka kwenye nyasi kando ya mto. 4 Kut 15:20;Hes 26:59Dada yake mtoto akasimama mbali ili ajue yatakayompata. 5 Mdo 7:21Basi binti Farao akashuka, aoge mtoni, na vijakazi wake wakatembea kando ya mto; naye akakiona kile kikapu katika nyasi, akamtuma kijakazi wake kwenda kukileta. 6 Akakifungua, akamwona mtoto, na tazama, mtoto yule analia. Basi akamhurumia, akasema, Huyu ni mmojawapo wa watoto wa Waebrania. 7 Basi dada yake mtoto akamwambia binti Farao, Je! Niende nikamwite mlezi katika wanawake wa Kiebrania, aje kwako, akunyonyeshee mtoto huyu? 8 Binti Farao akamwambia, Haya! Nenda. Yule kijana akaenda akamwita mama yake yule mtoto. 9 Binti Farao akamwambia, Mchukue mtoto huyu, ukaninyonyeshee, nami nitakupa mshahara wako. Yule mwanamke akamtwaa mtoto, akamnyonyesha. 10 Mdo 7:21Mtoto akakua, naye akamleta kwa binti Farao, akawa mwanawe. Akamwita jina lake Musa.2:10 Jina hili Musa katika Kiebrania ni ‘Mosheh’. Linatokana na neno ‘mashah’ kwa maana ya ‘kutoa’. Katika lugha ya Kimisri neno Musa ni ‘kupata mtoto’, akasema, Kwa sababu nilimtoa majini.