3 Na alipokuwa hawezi kumficha tena, akamtengenezea kikapu cha mafunjo akakitaliza kwa sifa na lami, akamtia mtoto ndani yake, akakiweka kwenye nyasi kando ya mto. 7 Basi dada yake mtoto akamwambia binti Farao, Je! Niende nikamwite mlezi katika wanawake wa Kiebrania, aje kwako, akunyonyeshee mtoto huyu? 8 Binti Farao akamwambia, Haya! Nenda. Yule kijana akaenda akamwita mama yake yule mtoto. 9 Binti Farao akamwambia, Mchukue mtoto huyu, ukaninyonyeshee, nami nitakupa mshahara wako. Yule mwanamke akamtwaa mtoto, akamnyonyesha.
Kutoka 2:3,7-9
Em outras traduções
- ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas
3 Lakini alipoona hawezi kuendelea kumficha, akamtengenezea kisafina cha mafunjo, akakipaka lami. Kisha akamweka huyo mtoto ndani yake, akakificha kwenye matete kando ya ukingo wa Mto Naili.
7 Ndipo dada wa huyo mtoto akamuuliza binti Farao, "Je, niende nikakutafutie mmoja wa wanawake wa Waebrania akulelee huyu mtoto?"
8 Binti Farao akamjibu, "Ndiyo, nenda." Yule msichana akaenda akamleta mama wa mtoto. 9 Binti Farao akamwambia, "Mchukue huyu mtoto unisaidie kumlea, nami nitakulipa." Basi yule mwanamke akamchukua mtoto na kumlea.
- ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli
3 Lakini alipoona hawezi kumficha zaidi, akamtengenezea kisafina cha mafunjo, akakipaka lami. Kisha akamweka huyo mtoto ndani yake, akakificha katikati ya matete kando ya ukingo wa Mto Naili.
7 Ndipo dada wa huyo mtoto akamuuliza binti Farao, "Je, niende nikakutafutie mmoja wa wanawake wa Kiebrania akulelee huyu mtoto?"
8 Binti Farao akamjibu, "Ndiyo, nenda." Yule msichana akaenda akamleta mama wa mtoto. 9 Binti Farao akamwambia, "Mchukue huyu mtoto unisaidie kumlea, nami nitakulipa." Basi yule mwanamke akamchukua mtoto na kumlea.
Direitos das traduções citadas
Estes versículos te tocaram? Ore agora!
+581 estão orando agora.
Junte-se à corrente de oração.