3 Kum 6:14;2 Fal 17:35;Yer 25:6Usiwe na miungu mingine ila mimi.
4 Kut 34:17;Law 19:4;26:1;Kum 4:15-18;27:15Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu chochote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. 5 Kut 34:6-7;Hes 14:18;Kum 7:9-10;Yos 23:7;24:19;2 Fal 17:35;Isa 44:15;Nah 1:2;Isa 14:20;Yer 2:9;Eze 18:19Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, 6 Zab 89:34;Rum 11:28;Kum 7:9nami nawarehemu maelfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.
7 Law 19:12;Zab 15:4;Mt 5:33;Mik 6:11Usilitaje bure jina la BWANA, Mungu wako, maana BWANA hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure.
8 Kut 16:23-30;31:12-14;Kum 5:12Ikumbuke siku ya Sabato uitakase. 9 Kut 23:12;31:15;34:21;35:2;Law 23:3;Lk 13:14Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; 10 Mwa 2:2;Neh 13:16lakini siku ya saba ni Sabato ya BWANA, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yoyote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. 11 Mwa 2:1-3;Kut 31:17Maana, kwa siku sita BWANA alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo BWANA akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa.
12 Kum 5:16;27:16;Yer 35:7,8;Mt 15:4;19:19;Mk 7:10;10:19;Lk 18:20;Efe 6:2-3;Law 19:3Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako.
13 Mwa 9:6;Law 24:17;Mt 5:21;19:18;Mk 10:19;Lk 18:20;Rum 13:9;Yak 2:11Usiue.
14 Law 20:10;Mt 5:27;19:18;Mk 10:19;Lk 18:20;Rum 13:9;Yak 2:11Usizini.
15 Law 19:11;1 The 4:6;Mt 19:18;Mk 10:19;Lk 18:20;Rum 13:9Usiibe.
16 Kut 23:1;Mt 19:18;Mk 10:19;Lk 18:20Usimshuhudie jirani yako uongo.
17 Rum 7:7;13:9;Mik 2:2;Efe 5:3;Mit 6:29;Mt 5:28Usiitamani nyumba ya jirani yako, usimtamani mke wa jirani yako; wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng’ombe wake, wala punda wake, wala chochote alicho nacho jirani yako.