Pazia
31 Law 16:2;2 Nya 3:14;Mt 27:51;Mk 15:38;Lk 23:45;Ebr 9:3Nawe fanya pazia la nyuzi za rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, na nguo za kitani nzuri zenye kusokotwa, litafumwa na kutiwa makerubi, kazi ya fundi stadi; 32 kisha litungike katika nguzo nne za mti wa mshita zilizofunikwa dhahabu, vifungo vyake vitakuwa vya dhahabu, katika vitako vya fedha vinne. 33 Ebr 6:19;9:3-5;Kut 25:16;40:21;Yos 4:11;1 Sam 4:6;6:19;1 Fal 8:6;1 Nya 15:1;Ufu 11:19;Law 16:2;Mt 24:15Nawe tungika lile pazia chini ya vile vifungo, nawe lete lile sanduku la ushuhuda na kulitia humo nyuma ya pazia; na lile pazia litawagawanyia kati ya patakatifu, na mahali patakatifu sana.