10 Zab 105:26;Mik 6:4Haya, basi, nitakutuma sasa kwa Farao, ili upate kuwatoa watu wangu, hao wana wa Israeli, katika Misri.
11 1 Sam 18:18;1 Fal 3:7-9;Isa 6:5,8;Yer 1:6Musa akamwambia Mungu, Mimi ni nani, hata niende kwa Farao, nikawatoe wana wa Israeli watoke Misri? 12 Mwa 31:3;Kum 31:23;Yos 1:5;Isa 43:2;Rum 8:31Akasema, Bila shaka mimi nitakuwa pamoja nawe; na dalili ya kuwa nimekutuma ndiyo hii; utakapokuwa umekwisha kuwatoa hao watu katika Misri, mtamwabudu Mungu katika mlima huu.