17 BWANA akanena na Musa, na kumwambia 18 Kut 38:8;1 Fal 7:38Fanya na birika la shaba, na kitako chake cha shaba, ili kuogea; nawe utaliweka kati ya hema ya kukutania na madhabahu, nawe utalitia maji. 19 Isa 52:11;Ebr 10:22Na Haruni na wanawe wataosha mikono yao na miguu yao humo; 20 hapo waingiapo ndani ya hema ya kukutania; watajiosha majini, ili wasife; au hapo watakapoikaribia madhabahu ili watumike, kumteketezea BWANA sadaka ya moto; 21 Kut 28:43basi wataosha mikono yao na miguu yao ili kwamba wasife; na neno hili litakuwa amri kwao milele, kwake yeye na kwa wazao wake katika vizazi vyao vyote.
Kutoka 30:17-21
Em outras traduções
- ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas
17 Kisha Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, 18 "Tengeneza sinia la shaba lenye kitako cha shaba kwa ajili ya kunawia. Liweke kati ya Hema la Kukutania na madhabahu, kisha uweke maji ndani yake. 19 Haruni na wanawe watanawa mikono na miguu yao kwa maji ya hilo sinia. 20 Wakati wowote wanapoingia katika Hema la Kukutania, watanawa kwa maji ili wasije wakafa. Pia, wanapokaribia madhabahu ili kuhudumu kwa kuleta sadaka zilizotolewa kwa Mwenyezi Mungu kwa moto, 21 watanawa mikono na miguu yao ili wasije wakafa. Hili litakuwa agizo la kudumu kwa Haruni na wazao wake kwa vizazi vijavyo."
- ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli
17 Kisha Bwana akamwambia Mose, 18 "Tengeneza sinia la shaba lenye kitako cha shaba kwa ajili ya kunawia. Liweke kati ya Hema la Kukutania na madhabahu, kisha uweke maji ndani yake. 19 Aroni na wanawe watanawa mikono na miguu yao kwa maji yatokayo katika hilo sinia. 20 Wakati wowote wanapoingia katika Hema la Kukutania, watanawa kwa maji ili kwamba wasije wakafa. Pia, wanapokaribia madhabahu ili kuhudumu kwa kuleta sadaka zilizotolewa kwa Bwana kwa moto, 21 watanawa mikono na miguu yao ili kwamba wasije wakafa. Hii itakuwa ni amri ya kudumu kwa ajili ya Aroni na wazao wake kwa vizazi vijavyo."
Direitos das traduções citadas
Estes versículos te tocaram? Ore agora!
+581 estão orando agora.
Junte-se à corrente de oração.