Pular para o conteúdo
Publicidade

Kutoka 31

Bezaleli na Oholiabu

1 BWANA akanena na Musa, na kumwambia, 2 Kut 35:30;1 Nya 2:20Angalia, nimemwita kwa jina lake Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila la Yuda; 3 Kut 35:31;1 Fal 7:14;Isa 28:26;1 Kor 12:4-8nami nimemjaza Roho ya Mungu, katika hekima, na maarifa, na ujuzi, na mambo ya kazi ya kila aina, 4 ili abuni kazi za ustadi, kuwa fundi wa dhahabu, na wa fedha, na wa shaba, 5 na kukata vito kwa kutiwa mahali, na kuchora miti, na kufanya kazi ya ustadi iwayo yote.

Veja também