Pular para o conteúdo
Publicidade

Kutoka 8:16-19

SRUV Swahili Revised Union Version

16 BWANA akamwambia Musa, Mwambie Haruni, Nyosha fimbo yako, ukayapige mavumbi ya nchi, ili kwamba yawe chawa katika nchi yote ya Misri. 17 Zab 105:31Nao wakafanya hivyo; Haruni akaunyosha mkono wake na fimbo yake, na kuyapiga mavumbi ya nchi, nayo yakawa chawa juu ya wanadamu na juu ya wanyama; mavumbi yote ya nchi yakawa ni chawa katika nchi yote ya Misri. 18 Kut 7:11;Lk 10:18;2 Tim 3:8,9Hao waganga nao wakafanya mfano wa hayo kwa uganga wao, ili kwamba walete chawa, lakini wasiweze; nako kulikuwa na chawa juu ya wanadamu, na juu ya wanyama. 19 Lk 11:20;1 Sam 6:3,9;Ayu 27:11;Zab 8:3;Mt 12:28;Mdo 13:11Ndipo wale waganga wakamwambia Farao, Jambo hili ni kidole cha Mungu;8:19 Katika Kiebrania ina maana ya ‘Nguvu ya Kimungu’ au ‘mkono wa Mungu’. na moyo wake Farao ukawa mgumu asiwasikize; vile vile kama BWANA alivyonena.

Baa la nne: Inzi

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    16 Ndipo Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, "Mwambie Haruni, ‘Nyoosha fimbo yako uyapige mavumbi ya ardhi,’ nayo nchi yote ya Misri mavumbi yatakuwa viroboto." 17 Wakafanya hivyo, Haruni aliponyoosha mkono wake wenye fimbo na kuyapiga mavumbi ya nchi, viroboto wakawajia watu na wanyama. Mavumbi yote katika nchi ya Misri yakawa viroboto. 18 Lakini waganga walipojaribu kutengeneza viroboto kwa siri ya uganga wao, hawakuweza. Nao viroboto walikuwa juu ya watu na wanyama.

    19 Waganga wale wakamwambia Farao, "Hiki ni kidole cha Mungu." Lakini moyo wa Farao ukawa mgumu naye hakuwasikiliza, kama vile Mwenyezi Mungu alivyokuwa amesema.

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    16 Ndipo Bwana akamwambia Mose, "Mwambie Aroni, ‘Nyoosha fimbo yako uyapige mavumbi ya ardhi,’ nayo nchi yote ya Misri mavumbi yatakuwa viroboto." 17 Wakafanya hivyo, Aroni aliponyoosha mkono wake wenye fimbo na kuyapiga mavumbi ya nchi, viroboto wakawajia watu na wanyama. Mavumbi yote katika nchi ya Misri yakawa viroboto. 18 Lakini waganga walipojaribu kutengeneza viroboto kwa siri ya uganga wao, hawakuweza. Nao viroboto walikuwa juu ya watu na wanyama.

    19 Waganga wale wakamwambia Farao, "Hiki ni kidole cha Mungu." Lakini moyo wa Farao ukawa mgumu naye hakuwasikiliza, kama vile Bwana alivyosema.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.