Pular para o conteúdo
Publicidade

Kutoka 9:8-11

SRUV Swahili Revised Union Version

8 BWANA akawaambia Musa na Haruni, Jitwalieni konzi za majivu ya tanuri, kisha Musa ayarushe juu kuelekea mbinguni mbele ya Farao. 9 Ufu 16:2Nayo yatakuwa ni mavumbi membamba juu ya nchi yote ya Misri, nayo yatakuwa majipu yenye kufura na kutumbuka juu ya wanadamu na juu ya wanyama, katika nchi yote ya Misri. 10 Ufu 16:2Basi wakatwaa majivu ya tanuri, na kusimama mbele ya Farao; na Musa akayarusha juu mbinguni nayo yakawa ni majipu yenye kufura na kutumbuka juu ya wanadamu na juu ya wanyama. 11 2 Tim 3:9Nao wale waganga hawakuweza kusimama mbele ya Musa kwa sababu ya hayo majipu, kwa maana hao waganga walikuwa na majipu, na Wamisri wote walikuwa nayo.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    8 Kisha Mwenyezi Mungu akamwambia Musa na Haruni, "Chukueni majivu ya tanuru, naye Musa ayarushe angani mbele ya Farao. 9 Yatakuwa vumbi jepesi juu ya nchi yote ya Misri, pia yatatokea majipu yenye kufura kwenye miili ya watu na ya wanyama katika nchi yote."

    10 Basi wakachukua majivu kwenye tanuru na kusimama mbele ya Farao. Musa akayarusha hewani, nayo majipu yenye kufura yakatokea kwenye miili ya watu na ya wanyama. 11 Waganga hawakuweza kusimama mbele ya Musa kwa sababu ya majipu yaliyokuwa kwenye miili yao, na kwenye miili ya Wamisri wote.

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    8 Kisha Bwana akamwambia Mose na Aroni, "Chukueni majivu ya tanuru, naye Mose ayarushe angani mbele ya Farao. 9 Yatakuwa vumbi jepesi juu ya nchi yote ya Misri, pia yatatokea majipu yenye kufura juu ya watu na wanyama katika nchi yote."

    10 Basi wakachukua majivu kwenye tanuru na kusimama mbele ya Farao. Mose akayarusha hewani, nayo majipu yenye kufura yakatokea miilini mwa watu na wanyama. 11 Waganga hawakuweza kusimama mbele ya Mose kwa sababu ya majipu yale yaliyokuwa miilini mwao na juu ya miili ya Wamisri wote.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.