14 Mwa 13:8;17:27;15:3;Mhu 2:7;Kum 34:1;Amu 18:29;Isa 41:2Abramu aliposikia ya kwamba nduguye amechukuliwa mateka, akawapa silaha vijana wake, waliozaliwa katika nyumba yake, watu mia tatu na kumi na wanane, akawafuata mpaka Dani. 15 Akajipanga apigane nao usiku, yeye na watumwa wake, akawapiga, akawafukuza mpaka Hoba, ulioko upande wa kushoto wa Dameski. 16 1 Sam 30:8,18,19Naye akarudisha mali zote, akamrudisha Lutu nduguye na mali zake, na wanawake pia, na watu.
18 Ebr 7:1-10;Zab 110:4;Mik 6:6;Mdo 16:17;Ebr 7:10-22Na Melkizedeki mfalme wa Salemu akaleta mkate na divai, naye alikuwa kuhani wa Mungu Aliye Juu Sana. 19 Akambariki, akasema, Abramu na abarikiwe na Mungu Aliye Juu Sana, Muumba mbingu na nchi. 20 Ebr 7:4Ahimidiwe Mungu Aliye Juu Sana, aliyewatia adui zako mikononi mwako. Abramu akampa fungu la kumi la vitu vyote.