14 Abramu alipopata habari kwamba jamaa yake amechukuliwa mateka, akawaita watu mia tatu na kumi na nane (318) wa nyumbani mwake waliokuwa wamefunzwa kupigana vita, wakawafuatilia hadi Dani. 15 Wakati wa usiku, Abramu aliwapanga watu wake katika vikosi, wakawashambulia na kuwashinda, wakawafukuza hadi Hoba, kaskazini mwa Dameski. 16 Abramu akarudisha mali yote, na akamrudisha Lutu jamaa yake na mali yake, pamoja na wanawake na watu wengine.
18 Ndipo Melkizedeki mfalme wa Salemu akaleta mkate na divai. Alikuwa kuhani wa Mungu Aliye Juu Sana. 19 Naye akambariki Abramu, akisema,
"Abarikiwe Abramu na Mungu Aliye Juu Sana,
Muumba wa mbingu na nchi.
20 Abarikiwe Mungu Aliye Juu Sana,
ambaye amewaweka adui zako mkononi mwako."
Ndipo Abramu akampa Melkizedeki sehemu ya kumi ya kila kitu.