Pular para o conteúdo
Publicidade

Hebreus 3

Musa ni mtumishi, Kristo ni Mwana

1 Ebr 4:14 Kwa hiyo, ndugu watakatifu, wenye kuushiriki mwito wa mbinguni, mtafakarini sana Mtume na Kuhani Mkuu wa maungamo yetu, Yesu, 2 Hes 12:7 aliyekuwa mwaminifu kwake yeye aliyemweka, kama Musa naye alivyokuwa, katika nyumba yote ya Mungu. 3 Kwa maana huyo amehesabiwa kuwa amestahili utukufu zaidi kuliko Musa, kama vile yeye aitengenezaye nyumba alivyo na heshima zaidi ya hiyo nyumba. 4 Maana kila nyumba imetengenezwa na mtu; ila yeye aliyevitengeneza vitu vyote ni Mungu. 5 Hes 12:7 Na Musa kweli alikuwa mwaminifu katika nyumba yote ya Mungu kama mtumishi, awe ushuhuda wa mambo yatakayonenwa baadaye; 6 Efe 2:19;Kol 1:23 bali Kristo, kama mwana, juu ya nyumba ya Mungu; ambaye nyumba yake ni sisi, kama tukishikamana sana na ujasiri wetu na fahari ya tumaini letu mpaka mwisho.

Onyo juu ya kutoamini

7 Zab 95:7-11 Kwa hiyo, kama anenavyo Roho Mtakatifu,

Leo, kama mkisikia sauti yake,

8 Kut 17:7;Hes 20:2-5 Msifanye mioyo yenu kuwa migumu,

Kama wakati wa kuasi,

Siku ya kujaribiwa katika jangwa,

9 Hapo baba zenu waliponijaribu, wakanipima,

Wakaona matendo yangu miaka arubaini.

10 Kwa hiyo nilichukizwa na kizazi hiki,

Nikasema, Sikuzote ni watu waliopotoka mioyo hawa;

Hawakuzijua njia zangu;

11 Hes 14:21-23 Kama nilivyoapa kwa hasira yangu,

Hawataingia rahani mwangu.

12 Hadharini, ndugu zangu, usiwepo katika mmoja wenu moyo mbovu wa kutoamini, ujitengao na Mungu aliye hai. 13 1 The 5:11 Lakini mwonyane kila siku, maadamu inaitwa leo; ili mmoja wenu asifanywe mgumu kwa udanganyifu wa dhambi. 14 Ebr 6:11;11:1 Kwa maana tumekuwa washirika wa Kristo, kama tukishikamana na mwanzo wa uthabiti wetu kwa nguvu mpaka mwisho; 15 Zab 95:7-8 kama inenwavyo,

Leo, kama mkisikia sauti yake,

Msifanye mioyo yenu kuwa migumu,

Kama wakati wa kuasi.

16 Hes 14:1-35;Kut 17:1 Maana ni akina nani walioasi, waliposikia? Si wale wote waliotoka Misri wakiongozwa na Musa? 17 Hes 14:29;1 Kor 10:10 Tena ni akina nani aliochukizwa nao miaka arubaini? Si wale waliokosa, ambao mizoga yao ilianguka katika jangwa? 18 Hes 14:22,23 Tena ni akina nani aliowaapia ya kwamba hawataingia katika pumziko lake, ila wale walioasi? 19 Basi twaona ya kuwa hawakuweza kuingia kwa sababu ya kutoamini kwao.

Veja também