Publicidade

Jeremias 30

Israeli na Yuda waahidiwa kurudishwa

1 Neno hili ndilo lililomjia Yeremia, kutoka kwa BWANA, kusema, 2 Isa 30:8 BWANA Mungu wa Israeli, asema hivi, ya kwamba, Uyaandike kitabuni maneno hayo yote niliyokuambia. 3 Kum 30:3;Amo 9:14;Yer 27:22;29:14;31:23;16:15 Kwa maana, tazama, siku zinakuja, asema BWANA, nitakapowarejesha watu wangu wa Israeli na Yuda waliofungwa, asema BWANA; nami nitawarudisha hadi katika nchi niliyowapa baba zao, nao wataimiliki.

4 Na haya ndiyo maneno aliyosema BWANA, kuhusu Israeli, na kuhusu Yuda. 5 Maana BWANA asema hivi, Tumesikia sauti ya tetemeko, na ya hofu, wala si ya amani. 6 Ulizeni sasa, mkaone kwamba mwanamume aona uchungu wa uzazi; mbona, basi, ninaona kila mtu anaweka mikono yake viunoni, kama mwanamke aliye na uchungu, na nyuso zote zimegeuka rangi? 7 Isa 23:4,5;Yoe 2:11;Amo 5:18;Sef 1:14;1 The 4:16;Dan 12:1 Ole! Maana siku ile ni kuu, hata hapana inayofanana nayo, maana ni wakati wa taabu yake Yakobo; lakini ataokolewa kutoka kwayo. 8 Na itakuwa katika siku ile, asema BWANA wa majeshi, nitaivunja nira yake itoke shingoni mwako, nami nitavipasua vifungo vyako; wala wageni hawatamtumikisha tena; 9 Isa 55:3,4;Hos 3:5;Lk 1:69;Mdo 2:30 bali watamtumikia BWANA, Mungu wao, na Daudi, mfalme wao, nitakayemwinua kwa ajili yao. 10 Yer 46:27-28 Kwa sababu hiyo usiogope, Ee Yakobo, mtumishi wangu, asema BWANA; wala usifadhaike, Ee Israeli; kwa maana, tazama, nitakuokoa toka mbali, na wazao wako toka nchi ya uhamisho wao; na Yakobo atarudi, naye atatulia na kustarehe, wala hapana mtu atakayemtia hofu. 11 Maana mimi ni pamoja nawe, asema BWANA, nikuokoe; maana nitawakomesha kabisa mataifa yote huko nilikokutawanya, bali sitakukomesha wewe kabisa; lakini nitakurudi kwa hukumu, wala sitakuacha bila adhabu.

12 2 Nya 36:16;Yer 15:18 Maana BWANA asema hivi, Maumivu yako hayaponyeki, na jeraha lako ni kubwa. 13 Hapana mtu wa kukutetea; kwa jeraha lako huna dawa ziponyazo. 14 Omb 1:2;Yer 5:6;Ayu 13:24;30:21 Wote wakupendao wamekusahau; hawakutafuti; maana nimekujeruhi kwa jeraha la adui, kwa adhabu ya mtu mkatili; kwa sababu ya ukubwa wa uovu wako, kwa sababu dhambi zako zilikuwa zimeongezeka. 15 Mbona unalilia maumivu yako? Maumivu yako hayaponyeki; kwa sababu ya ukubwa wa uovu wako, kwa sababu dhambi zako zimeongezeka, nimekutenda haya. 16 Kut 23:22;Isa 41:11 Basi, watu wote wakulao wataliwa; na adui zako wote watakwenda kufungwa; kila mmoja wao; na hao waliokuteka nyara watatekwa; na wote waliokuwinda nitawafanya kuwa mawindo. 17 Kut 15:26;Isa 30:26;Hos 6:2;Mal 4:2;1 Pet 2:24 Maana nitakurudishia afya, nami nitakuponya majeraha yako, asema BWANA, kwa sababu wamekuita, mwenye kutupwa, wakisema, Ni Sayuni, mji ambao hakuna mtu autakaye. 18 Zab 102:13 BWANA asema hivi, Tazama, nitarudisha tena hema za Yakobo zilizohamishwa, na kuyahurumia makao yake; nao mji huo utajengwa juu ya magofu yake wenyewe, nalo jumba litakaliwa, kama ilivyokuwa desturi yake. 19 Ezr 3:10,11;Neh 8:12;Isa 35:10;Zek 10:8 Tena kwao itasikiwa shukrani, na sauti yao wachangamkao; nami nitawazidisha, wala hawatakuwa wachache; tena nitawatukuza, wala hawatakuwa wanyonge. 20 Isa 1:26 Watoto wao nao watakuwa kama zamani, na kusanyiko lao litathibitika mbele zangu, nami nitawaadhibu wote wanaowaonea. 21 Mwa 49:10;Hes 16:5 Na mkuu wao atakuwa mtu wa kwao wenyewe, naye mwenye kuwatawala atakuwa mtu wa jamaa yao; nami nitamkaribisha, naye atanikaribia; maana ni nani aliye na moyo wa kuthubutu kunikaribia? Asema BWANA. 22 Nanyi mtakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wenu.

23 Yer 25:32 Tazama, tufani ya BWANA, yaani, ghadhabu yake, imetokea tufani ya kudumu; itawaangukia waovu vichwani. 24 Hasira kali ya BWANA haitarudi, hadi atakapokwisha kutenda na kuyatimiza makusudi ya moyo wake; katika siku za mwisho mtayafahamu haya.

Veja também

Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_12-11-46-