31 Yer 32:40;33:14;Ebr 8:8;Mt 26:28;Mk 14:24;Lk 22:20;1 Kor 11:25;2 Kor 3:6;Ebr 8:8-12Angalia, siku zinakuja, asema BWANA, nitakapofanya agano jipya na nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda.
Agano jipya
32 Yn 1:17;Kum 1:31Si kwa mfano wa agano lile nililolifanya na baba zao, katika siku ile nilipowashika mkono, ili kuwatoa katika nchi ya Misri; ambalo agano langu hilo walilivunja, ingawa nilikuwa mume kwao, asema BWANA. 33 Yer 32:40;24:7;30:22;Zab 40:8;2 Kor 3:3;Ebr 10:16Bali agano hili ndilo nitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya siku zile, asema BWANA; Nitatia sheria yangu ndani yao, na katika mioyo yao nitaiandika; nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.