Pular para o conteúdo
Publicidade

Levítico 18

6 Mtu yeyote miongoni mwenu asimkaribie mwenziwe aliye wa jamaa yake ya karibu ili kumfunua utupu; mimi ndimi BWANA. 7 Utupu wa baba yako, wala utupu wa mama yako, usifunue, maana ndiye mama yako; usifunue utupu wake. 8 Law 20:11;Kum 22:30;27:20;Mwa 49:4;1 Kor 5:1Utupu wa mke wa baba yako, usifunue; maana, ni utupu wa baba yako. 9 Law 20:17;Kum 27:22;2 Sam 13:12Utupu wa dada yako, binti ya baba yako, au binti ya mama yako, awe alizaliwa nyumbani mwenu au kwingine, utupu wa hao usifunue. 10 Utupu wa binti ya mwanao wa kiume, au wa binti ya binti yako, utupu wao hao usifunue; kwa kuwa ni utupu wako mwenyewe. 11 Utupu wa binti ya mkewe baba yako, aliyezaliwa na baba yako, yeye ni dada yako, usifunue utupu wake. 12 Law 20:19-20Usifunue utupu wa dada ya baba yako; maana, yeye ni jamaa wa karibu. 13 Usifunue utupu wa dada ya mama yako; maana, yeye ni jamaa ya mama yako wa karibu. 14 Usifunue utupu wa ndugu ya baba yako, usimkaribie mkewe huyo; yeye ni shangazi yako. 15 Law 20:12;Mwa 38:18;Eze 22:11Usifunue utupu wa mkweo mwanamke; yeye ni mke wa mwanao; usifunue utupu wake huyo. 16 Law 20:21;Mt 14:3,4;22:24Usifunue utupu wa mke wa nduguyo; maana, ni utupu wa nduguyo. 17 Law 20:14;Kum 27:23Usifunue utupu wa mwanamke na binti yake; usimtwae binti ya mwanaye wa kiume, au binti ya binti yake, ili kufunua utupu wake; hao ni jamaa ya karibu; ni uovu mkuu. 18 Mwa 30:15;Mal 2:15Wala usitwae18:18 Au usimuoe. mwanamke pamoja na dada yake, awe mtesi wake, na kufunua utupu wake, dada yake akiwa hai. 19 Law 20:18;Eze 18:6Usimwendee mwanamke kufunua utupu wake atakapokuwa najisi kwa ajili ya hedhi. 20 Law 20:10;Mit 6:29;Mal 3:5;Mt 5:27,28;1 Kor 6:9;Ebr 13:4Usilale na mke wa mwenzio, ukajitia unajisi naye. 21 Law 20:1-5;2 Fal 16:3;Yer 19:5;1 Fal 11:7,33;Eze 36:20;Mal 1:12;Isa 42:8Usimtoe kafara mzawa wako yeyote kwa Moleki18:21 Moleki ni jina la mungu aliyeabudiwa na Wakanaani, kwa kutoa dhabihu ya watoto wao kwa kuwapitisha motoni. Katika Agano Jipya ni Moloki. na ulinajisi jina la Mungu wako; mimi ndimi BWANA. 22 Law 20:13;Rum 1:27;1 Tim 1:10Usilale na mwanamume mfano wa kulala na mwanamke; ni machukizo. 23 Kut 22:18;Law 20:15-16;Kum 27:21Wala usilale na mnyama yeyote, ili kujitia unajisi kwake; wala mwanamke asisimame mbele ya mnyama ili kulala naye; ni upotovu.

Veja também