Kuhusu kujilipiza kisasi
38 Kut 21:24;Law 24:20;Kum 19:21Mmesikia kwamba imenenwa, Jicho kwa jicho, na jino kwa jino; 39 Lk 6:27-36Lakini mimi nawaambia, Msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akupigaye shavu la kulia, mgeuzie na la pili. Yn 18:22,23;Law 19:1840 1 Kor 6:7Na mtu atakaye kukushitaki na kulichukua shati lako, mwachie na koti pia. 41 Mtu yeyote akikulazimisha mwendo wa maili moja, nenda naye maili mbili. 42 Akuombaye, mpe; naye atakaye kukopa kwako, usimpe kisogo.