38 "Mmesikia kwamba ilinenwa, ‘Jicho kwa jicho na jino kwa jino.’ 39 Lakini mimi nawaambia, msishindane na mtu mwovu. Lakini kama mtu akikupiga kwenye shavu la kuume, mgeuzie na la pili pia. 40 Mtu akitaka kukushtaki na kuchukua joho lako, mwachie achukue na koti pia. 41 Mtu akikulazimisha kwenda maili moja5:41 kama kilomita 1.6, nenda naye maili mbili5:41 kama kilomita 3.2. 42 Mpe yeye akuombaye, wala usimgeuzie kisogo yeye atakaye kukukopa.
Wapendeni adui zenu
(Luka 6:27-28, 32-36)