33 Kut 3:2;Kum 1:33;Yer 31:2Basi wakasafiri kutoka penye mlima wa BWANA safari ya siku tatu; na sanduku la Agano la BWANA likatangulia mbele yao mwendo wa siku tatu, ili kuwatafutia mahali pa kupumzika. 34 Kut 13:21;Neh 9:12,19;Zab 105:39Na wingu la BWANA lilikuwa juu yao mchana hapo waliposafiri kwenda mbele kutoka kambini.
35 Zab 68:1,2;Isa 51:9Ilikuwa, hapo sanduku liliposafiri kwenda mbele, ndipo Musa akasema, Inuka, Ee BWANA, adui zako na watawanyike; na wakimbie mbele zako hao wakuchukiao. 36 Zab 90:14,17;132:8Tena hapo liliposimama, akasema, Ee BWANA, uwarudie maelfu kumi ya maelfu ya Israeli.10:36 Au Rudi Ee BWANA wa maelfu na maelfu ya Israeli.