Familia ya Elimeleki yaenda Moabu
1 Amu 2:16;Mwa 12:10;26:1;Kum 28:38;1 Fal 18:2;2 Fal 8:1;Amu 17:8;Mik 5:2 Hapo zamani Waamuzi walipokuwa wanatawala, njaa ilitokea katika nchi. Mtu mmoja wa Bethlehemu ya Yuda, akaondoka akaenda kukaa katika nchi ya Moabu, yeye na mkewe na wanawe wawili. 2 Mwa 35:19;Amu 3:30 Na jina la mtu huyo aliitwa Elimeleki,1:2 Elimeleki: maana yake ni ‘Mungu ni Mfalme’. 1:2 Naomi: maana yake ni ‘Mwema’. 1:2 Maloni: maana yake ni ‘Ugonjwa’. 1:2 Kilioni: maana yake ni ‘Upotevu’. na jina la mkewe Naomi, na majina ya wanawe wawili Maloni na Kilioni, Waefrata wa Bethlehemu ya Yuda. Wakafika nchi ya Moabu, wakakaa huko. 3 Akafa Elimeleki, mumewe Naomi; na yule mwanamke akasalia na wanawe wawili. 4 Nao wakaoa wanawake wa Kimoabu, jina la mmoja aliitwa Orpa, na jina la wa pili Ruthu. Baada ya kukakaa huko miaka kumi hivi, 5 wote wawili Maloni na Kilioni wakafa; na huyo mwanamke akawa amefiwa na wanawe wawili, na mumewe pia.
Naomi na wakweze Wamoabi
6 Kut 4:31;Zab 80:14;Yer 29:10;Sef 2:7;Zek 10:3;Lk 1:68;7:16;Mwa 28:20;48:15;Kut 16:4,6;Zab 104:14,16;Mit 30:8;Isa 55:10;Mt 6:11 Ndipo alipoondoka, yeye na wakweze, ili kurudi kutoka nchi ya Moabu; maana akiwa katika nchi ya Moabu alipata habari kuwa BWANA alikuwa amewajia watu wake na kuwapa chakula. 7 Basi akatoka pale alipokuwa akiishi, na wakweze wawili pamoja naye; wakashika njia ili kurudi mpaka nchi ya Yuda. 8 Yos 24:15;2 Tim 1:16 Kisha Naomi akawaambia wakweze wawili, Nendeni sasa mkarejee kila mmoja nyumbani kwa mamaye; BWANA na awatendee mema ninyi, kama ninyi mlivyowatendea mema hao waliofariki na mimi pia. 9 Rut 3:1 BWANA na awajalie kuona raha kila mmoja nyumbani kwa mumewe. Kisha akawabusu; nao wakapaza sauti zao wakalia. 10 Wakamwambia, La, sivyo; lakini tutarudi pamoja nawe kwa watu wako. 11 Mwa 38:11;Kum 25:5 Naye Naomi akasema, Enyi wanangu, rudini; kwa nini mfuatane nami? Je! Mimi ninao watoto wa kiume tena tumboni mwangu, hata wawe waume zenu? 12 Enyi wanangu, mrejee; nendeni zenu; kwa kuwa mimi ni mzee, siwezi kupata mume tena. Kama ningesema, Natumaini; kama ningepata mume hata usiku huu, na kuzaa watoto wa kiume; 13 Amu 2:15;Ayu 19:21;Zab 32:4;38:2 je! Mngesubiri hata watakapokuwa watu wazima? Mngejizuia msiwe na waume? La, sivyo, wanangu; maana ni vigumu kwangu kuliko kwenu, kwa sababu mkono wa BWANA umetoka juu yangu. 14 Kum 4:4;10:20;Mit 17:17;18:24;Yn 6:66-69;Ebr 10:39 Nao wakapaza sauti zao, wakalia tena, na Orpa akambusu mkwewe, lakini Ruthu akaambatana naye. 15 Yos 24:15-21;Amu 11:24 Naye akasema, Tazama, dada yako amerudi kwa watu wake, na kwa mungu wake; basi urudi nawe ukamfuate dada yako. 16 Naye Ruthu akasema,
Usinisihi nikuache,
Nirudi nisifuatane nawe;
Maana wewe uendako nitakwenda,
Na wewe ukaapo nitakaa.
Watu wako watakuwa watu wangu,
Na Mungu wako atakuwa Mungu wangu;
17 1 Sam 3:17;25:25;2 Fal 6:31 Pale utakapofia ndipo nitakufa nami,
Na papo hapo nitazikwa;
BWANA anitende vivyo hivyo na kuzidi,
Ila kufa tu kutatutenga wewe nami.
18 Mdo 21:14 Basi alipomwona kuwa amekata shauri kufuatana naye, aliacha kumshawishi.
19 Mt 21:10;Isa 23:7;Omb 2:15 Hivyo hao wakaendelea wote wawili hadi walipofika Bethlehemu. Na ikawa walipofika Bethlehemu, mji wote uliwaajabia. Nao wanawake wakasema, Je! Huyu ni Naomi? 20 Akawaambia, Msiniite Naomi,1:20 Tazama Rut 1:2. niiteni Mara1:20 Mara: maana yake ni, ‘Uchungu’. kwa sababu Mwenyezi Mungu amenitenda mambo machungu sana. 21 1 Sam 2:7,8;Ayu 1:21 Mimi nilitoka nikiwa nimejaa, naye BWANA amenirudisha sina kitu, kwani kuniita Naomi, ikiwa BWANA ameshuhudia juu yangu, na Mwenyezi Mungu amenitesa? 22 Kut 9:31;2 Sam 21:9 Basi Naomi akarudi; pamoja na Ruthu Mmoabi, mkwewe; ambao walirudi kutoka nchi ya Moabu; nao wakafika Bethlehemu mwanzo wa mavuno ya shayiri.