Publicidade

Bom dia

Por Bíblia Online

Cada manhã é presente de Deus. As misericórdias do Senhor se renovam cada dia. A Bíblia convida a começar o dia com louvor, oração e gratidão ao Criador.

Manhã com Deus

De manhã te apresentarei a minha oração. Pela manhã ouvirás a minha voz — eu te busco ao despertar.

BWANA, asubuhi utaisikia sauti yangu,

Asubuhi nitakupangia dua yangu na kutazamia.

Lakini mimi nimekulilia Wewe, BWANA,

Na asubuhi maombi yangu yatakuwasilia.

Amka, ee moyo wangu.

Amka, kinanda na kinubi,

Nitaamka alfajiri.

Nami nitaimba juu ya nguvu zako,

Nitaimba kwa furaha juu ya fadhili zako asubuhi.

Maana umekuwa ngome yangu,

na kimbilio wakati wa mateso yangu.

Nami nitaimba juu ya nguvu zako,

Nitaimba kwa furaha juu ya fadhili zako asubuhi.

Maana umekuwa ngome yangu,

na kimbilio wakati wa mateso yangu.

Ee nguvu zangu, nitakuimbia sifa,

Maana Ewe Mungu ndiwe ngome yangu,

Mungu wa fadhili zangu.

Uniwezeshe kusikia fadhili zako asubuhi,

Kwa maana nimekutumaini Wewe.

Unifundishe njia nitakayoiendea,

Kwa maana ninakuinulia nafsi yangu.

Bali mimi nikutazame uso wako katika haki,

Niamkapo nishibishwe kwa sura yako.

Misericórdias renovadas

As misericórdias do Senhor se renovam cada manhã. Este é o dia que o Senhor fez — alegremo-nos e nos regozijemos nele.

Ni huruma za BWANA kwamba hatuangamii,

Kwa kuwa rehema zake hazikomi.

Ni mpya kila siku asubuhi;

Uaminifu wako ni mkuu.

BWANA ndiye fungu langu, husema nafsi yangu,

Kwa hiyo nitamtumaini yeye.

Ni huruma za BWANA kwamba hatuangamii,

Kwa kuwa rehema zake hazikomi.

Ni mpya kila siku asubuhi;

Uaminifu wako ni mkuu.

Siku hii ndiyo aliyoifanya BWANA,

Tutashangilia na kuifurahia.

Mwimbieni BWANA zaburi,

Enyi watauwa wake.

Na kutoa shukrani.

Kwa kukumbuka utakatifu wake.

Maana ghadhabu zake ni za muda mfupi tu;

Radhi yake ni ya milele.

Kilio huweza kuwapo usiku,

Lakini furaha huja asubuhi.

Maana ghadhabu zake ni za muda mfupi tu;

Radhi yake ni ya milele.

Kilio huweza kuwapo usiku,

Lakini furaha huja asubuhi.

Kwa hiyo wakaao mbali kabisa huogopa ishara zako;

Milango ya asubuhi na jioni waifurahisha.

Utushibishe asubuhi kwa fadhili zako,

Nasi tutashangilia na kufurahi siku zetu zote.

Louvor matinal

Saciai-nos de manhã com a tua benignidade. Todo dia te louvarei e celebrarei o teu nome para sempre.

Ukuu na wema wa Mungu

Ee Mungu wangu, Mfalme, nitakutukuza,

Nitalihimidi jina lako milele na milele.

Kila siku nitakuhimidi,

Nitalisifu jina lako milele na milele.

Shukrani kwa ajili ya uthibitisho

Ni neno jema kumshukuru BWANA,

Na kuliimbia jina lako sifa, Ee Uliye Juu.

Kuzitangaza rehema zako asubuhi,

Na uaminifu wako wakati wa usiku.

Sifa kwa Mungu atoaye hukumu

Mwimbieni BWANA wimbo mpya,

Mwimbieni BWANA, nchi yote.

Mwimbieni BWANA, lisifuni jina lake,

Tangazeni wokovu wake kila siku.

Wahubirieni mataifa habari za utukufu wake,

Na watu wote habari za maajabu yake.

* * *

Sheria yako naipenda mno ajabu,

Ndiyo kutafakari kwangu mchana kutwa.

Mchana BWANA ataagiza fadhili zake, na usiku wimbo wake utakuwa nami,

Naam, maombi kwa Mungu aliye uhai wangu.

Ee BWANA, uturehemu; tumekungoja wewe; uwe wewe mkono wetu kila asububi, na wokovu wetu pia wakati wa taabu.

Kuaibishwa na kuthibitishwa kwa mtumishi

Bwana MUNGU amenipa ulimi wa hao wafundishwao, nipate kujua jinsi ya kumtegemeza kwa maneno yeye aliyechoka, huniamsha asubuhi baada ya asubuhi; huniamsha, sikio langu lipate kusikia kama watu wafundishwao.

Graça para o novo dia

O Senhor te abençoe e te guarde. Cada novo dia é oportunidade de viver sob a graça do Deus que nos ama.

BWANA akubariki, na kukulinda;

BWANA akuangazie nuru za uso wake, na kukufadhili;

BWANA akuinulie uso wake, na kukupa amani.

Asubuhi panda mbegu zako,

Wala jioni usiulegeze mkono wako.

Kwa maana wewe hujui ni zipi zitakazofanikiwa, kama ni hii au hii, au kama zote zitafaa sawasawa.

Tena huamka, kabla usiku haujaisha;

Huwapa watu wa nyumbani mwake chakula;

Na wajakazi wake sehemu zao.

Usipende usingizi usije ukawa maskini;

Fumbua macho yako nawe utashiba chakula.

Mungu akaiona nuru, ya kuwa ni njema; Mungu akatenga nuru na giza. Mungu akaiita nuru Mchana, na giza akaliita Usiku. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya kwanza.

Nasi tuna lile neno la unabii lililo imara zaidi, ambalo, mkiliangalia, kama taa iangazayo mahali penye giza, mwafanya vyema, mpaka kutakapopambazuka, na nyota ya asubuhi kuzuka mioyoni mwenu.

ambaye alikufa kwa ajili yetu, ili tuishi pamoja naye, iwe tunakesha au tunalala.

Seja o primeiro
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_12-11-46-