Publicidade

Salmos 96

Sifa kwa Mungu atoaye hukumu

1 Mwimbieni BWANA wimbo mpya,

Mwimbieni BWANA, nchi yote.

2 Mwimbieni BWANA, lisifuni jina lake,

Tangazeni wokovu wake kila siku.

3 Wahubirieni mataifa habari za utukufu wake,

Na watu wote habari za maajabu yake.

4 Kwa kuwa BWANA ni mkuu mwenye kusifiwa sana.

Na wa kuhofiwa kuliko miungu yote.

5 Isa 41:24;Yer 10:11;Hab 2:18-20;Mdo 19:26;1 Kor 8:4,5;Mwa 1:1;Isa 42:5;Yer 10:11 Maana miungu yote ya watu si kitu,

Lakini BWANA ndiye aliyezifanya mbingu.

6 Heshima na adhama ziko mbele zake,

Nguvu na uzuri zimo katika patakatifu pake.

7 Zab 29:1-2 Mpeni BWANA, enyi jamaa za watu,

Mpeni BWANA utukufu na nguvu.

8 Mpeni BWANA utukufu wa jina lake,

Leteni sadaka, na mwingie katika nyua zake.

9 Mwabuduni BWANA kwa uzuri wa utakatifu,

Tetemekeni mbele zake, nchi yote.

10 Ufu 11:15;Yn 5:22 Semeni katika mataifa, BWANA ametamalaki;

Naam, ulimwengu umethibitika usitikisike,

Atawahukumu watu kwa adili.

11 Mbingu na zifurahi, nchi na ishangilie,

Bahari na ivume na vyote viijazavyo,

12 Mashamba na yashangilie, na vyote vilivyomo,

Ndipo miti yote ya mwituni iimbe kwa furaha;

13 Ufu 19:11 Mbele za BWANA, kwa maana anakuja,

Kwa maana anakuja aihukumu nchi.

Atauhukumu ulimwengu kwa haki,

Na mataifa kwa uaminifu wake.

Veja também

Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_12-11-46-