Kwa mwimbishaji: kwa mtindo wa Usiharibu. Utenzi wa Daudi alipomponyoka Sauli na kujificha pangoni.
1 Isa 26:20 Unirehemu, Ee Mungu, unirehemu mimi,
Maana nafsi yangu imekukimbilia Wewe.
Nitaukimbilia uvuli wa mbawa zako,
Hadi misiba hii itakapopita.
2 Zab 138:8 Nitamwita MUNGU Aliye Juu,
Mungu anitimiziaye mambo yangu.
3 Zab 144:5;40:11 Atanitumia msaada toka mbinguni na kuniokoa,
Atawaaibisha wale wanaotaka kunishambulia.
Mungu atazituma
Fadhili zake na kweli yake.
4 Mit 30:14;Zab 64:3 Nafsi yangu i kati ya simba,
Nitastarehe kati yao waliowaka moto.
Wanadamu meno yao ni mikuki na mishale,
Na ndimi zao ni upanga mkali.
5 Zab 108:5 Ee Mungu, utukuzwe juu ya mbingu,
Na juu ya nchi yote uwe utukufu wako.
6 Zab 9:15 Wameweka wavu ili kuninasa miguu;
Nimevunjika moyo;
Wamechimba shimo njiani mwangu;
Lakini wao wenyewe wametumbukia humo!
7 Zab 108:1 Ee Mungu, moyo wangu ni thabiti,
Moyo wangu ni thabiti.
Nitaimba, nitaimba kwa sauti nzuri,
8 Amu 5:12 Amka, ee moyo wangu.
Amka, kinanda na kinubi,
Nitaamka alfajiri.
9 Ee Bwana, nitakushukuru kati ya watu,
Nitakuimbia sifa kati ya mataifa.
10 Zab 108:4 Maana fadhili zako ni kubwa hata mbinguni,
Na uaminifu wako hata mawinguni.
11 Ee Mungu, utukuzwe juu ya mbingu,
Na juu ya nchi yote uwe utukufu wako.