Publicidade

Lamentações 3

Upendo wa Mungu huvumilia

1 Mimi ni mtu aliyeona mateso

Kwa fimbo ya ghadhabu yake.

2 Ameniongoza na kunipeleka katika giza

Wala si katika nuru.

3 Hakika juu yangu augeuza mkono wake

Mara kwa mara mchana wote.

4 Amechakaza ngozi yangu na nyama yangu;

Ameivunja mifupa yangu.

5 Amejenga boma juu yangu,

Na kunizungusha uchungu na uchovu.

6 Zab 88:5 Amenikalisha penye giza,

Kama watu waliokufa zamani.

7 Amenizinga pande zote hata siwezi kutoka;

Amenifunga kwa mnyororo mzito.

8 Ayu 30:20;Zab 22:2 Naam, nikilia na kuomba msaada,

Huyapinga maombi yangu.

9 Ameziziba njia zangu kwa mawe yaliyochongwa;

Ameyapotosha mapito yangu.

10 Hos 5:14 Alivyo kwangu ni kama dubu aoteaye,

Kama simba aliye mafichoni.

11 Hos 6:1 Amezigeuza njia zangu, na kuniraruararua;

Amenifanya ukiwa.

12 Ayu 6:4;Zab 34:2 Ameupinda upinde wake,

Na kunifanya niwe shabaha kwa mshale.

13 Amenichoma viuno

Kwa mishale ya podo lake.

14 Neh 4:2-4;Zab 22:6,7;Yer 20:7;Mt 27:29-31 Nimekuwa dhihaka kwa watu wangu wote;

Wimbo wao mchana kutwa.

15 Yer 9:15 Amenijaza uchungu,

Amenikinaisha kwa pakanga.

16 Mit 20:17 Amenivunja meno kwa changarawe;

Amenifunika majivu.

17 Umeniweka nafsi yangu mbali na amani;

Nikasahau kufanikiwa.

18 Zab 31:22 Nikasema, Nguvu zangu zimepotea,

Na tumaini langu kwa BWANA.

19 Kumbuka mateso yangu, na msiba wangu,

Pakanga na nyongo.

20 Nafsi yangu ingali ikiyakumbuka hayo,

Nayo imeinama ndani yangu.

21 Najikumbusha neno hili,

Kwa hiyo nina matumaini.

22 Neh 9:31;Zab 57:10;Mal 3:6 Ni huruma za BWANA kwamba hatuangamii,

Kwa kuwa rehema zake hazikomi.

23 Isa 33:2;Ebr 10:23 Ni mpya kila siku asubuhi;

Uaminifu wako ni mkuu.

24 Zab 16:5 BWANA ndiye fungu langu, husema nafsi yangu,

Kwa hiyo nitamtumaini yeye.

25 Zab 130:6 BWANA ni mwema kwa hao wamngojeao,

Kwa hiyo nafsi imtafutayo.

26 Zab 37:7 Ni vema mtu autarajie wokovu wa BWANA

Na kumngojea kwa utulivu.

27 Zab 90:12 Ni vema mwanadamu aichukue nira

Wakati wa ujana wake.

28 Yer 15:17 Na akae peke yake na kunyamaza kimya;

Kwa sababu Bwana ameweka hayo juu yake.

29 Ayu 42:6 Na atie kinywa chake mavumbini;

Ikiwa yamkini liko tumaini.

30 Mik 5:1;Mt 5:39 Na amwelekezee yule ampigaye shavu lake;

Ashibishwe mashutumu.

31 Zab 94:14 Kwa kuwa Bwana hatamtupa mtu

Hata milele.

32 Maana ajapomhuzunisha atamrehemu,

Kwa kadiri ya wingi wa huruma zake.

33 Ebr 12:10 Maana moyo wake hapendi kuwatesa wanadamu.

Wala kuwahuzunisha.

34 Wafungwa wote wa duniani

Kupondwa chini kwa miguu,

35 Kuipotosha hukumu ya mtu

Mbele zake Aliye Juu,

36 Hab 1:13 Na kumnyima mtu haki yake,

Hayo Bwana hayaridhii kabisa.

37 Zab 33:9 Ni nani asemaye neno nalo likafanyika,

Ikiwa Bwana hakuliagiza?

38 Ayu 2:10 Je! Katika kinywa chake Aliye Juu

Hayatoki maovu na mema?

39 Mik 7:9 Mbona anung’unika mwanadamu aliye hai

Mtu akiadhibiwa kwa dhambi zake?

40 Zab 119:59 Na tuchunguze njia zetu na kuzijaribu,

Na kumrudia BWANA tena.

41 Zab 86:4 Na tumwinulie Mungu aliye mbinguni

Mioyo yetu na mikono.

42 Dan 9:5 Sisi tumekosa na kuasi;

Wewe hukusamehe.

43 Umetufunika kwa hasira na kutufuatia;

Umeua, wala hukuona huruma.

44 Umejifunika nafsi yako kwa wingu,

Maombi yetu yasipite.

45 1 Kor 4:13 Umetufanya kuwa takataka, na vifusi

Katikati ya mataifa.

46 Juu yetu adui zetu wote

Wametupanulia vinywa vyao.

47 Hofu imetujilia na shimo,

Ukiwa na uharibifu.

48 Jicho langu lachuruzika mito ya machozi

Kwa sababu ya kuharibiwa kwa binti zangu.

49 Jicho langu latoka machozi lisikome,

Wala haliachi;

50 Isa 63:15 Hata BWANA atakapoangalia

Na kutazama toka mbinguni.

51 Jicho langu lanitia huzuni nafsini mwangu,

Kwa ajili ya kuangamizwa kwa binti wa watu wangu.

52 Zab 35:7;69:4 Walio adui zangu bila sababu

Wameniwinda sana kama ndege;

53 Yer 37:16;Dan 6:17 Wameukatilia mbali uhai wangu gerezani,

Na kutupa jiwe juu yangu.

54 Zab 69:2 Maji mengi yalipita juu ya kichwa changu,

Nikasema, Nimekatiliwa mbali.

55 2 Nya 33:12;Zab 18:5,6;Yon 2:2 Nililiitia jina lako, BWANA, kutoka lile shimo

Liendalo chini kabisa.

56 Zab 6:8;Rum 8:26 Ukaisikia sauti yangu; usifiche sikio lako

Ili usisikie pumzi yangu, kwa kilio changu.

57 Zab 69:18;Isa 58:9;Yak 4:8 Ulinikaribia siku ile nilipokulilia;

Ukasema, Usiogope.

58 1 Sam 25:39;Yer 51:36;Zab 35:1;71:23 Ee BWANA umenitetea katika kisa cha nafsi yangu;

Umeukomboa uhai wangu.

59 Umekuona kudhulumiwa kwangu, Ee BWANA;

Unihukumie neno langu.

60 Yer 11:19 Umekiona kisasi chao chote,

Na mashauri yao yote juu yangu.

61 Ee BWANA, umeyasikia matukano yao,

Na mashauri yao yote juu yangu;

62 Midomo yao walioinuka juu yangu

Na maazimio yao juu yangu mchana kutwa.

63 Zab 139:2 Uangalie kuketi kwao, na kuinuka kwao;

Wimbo wao ndio mimi.

64 Zab 28:4;Yer 11:20;2 Tim 4:14;Ufu 6:10 Utawalipa malipo, Ee BWANA,

Sawasawa na kazi ya mikono yao.

65 Zab 8:3 Utawapa ushupavu wa moyo;

Laana yako juu yao.

66 Utawafuatia kwa hasira, na kuwaangamiza

Wasiwe tena chini ya mbingu za BWANA.

Veja também

Lamentações
Ver todos os capítulos de Lamentações
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_19-25-13-