O que é bom
O que é bom vem de Deus. A Bíblia celebra a bondade divina e nos convida a discernir, praticar e desfrutar tudo o que é bom — porque toda boa dádiva vem do Pai das luzes.
Mungu akaona kila kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya sita.
BWANA yu mwema, mwenye adili,
Kwa hiyo atawafundisha wenye dhambi njia.
Nami kumkaribia Mungu ni kwema kwangu;
Nimefanya kimbilio kwa Bwana MUNGU,
Niyahubiri matendo yako yote.
Ni neno jema kumshukuru BWANA,
Na kuliimbia jina lako sifa, Ee Uliye Juu.
Kuzitangaza rehema zako asubuhi,
Na uaminifu wako wakati wa usiku.
Kwa chombo chenye nyuzi kumi,
Na kwa kinanda,
Na kwa mlio wa kinubi.
Maana BWANA ni mwema;
Rehema zake ni za milele;
Na uaminifu wake katika vizazi vyote.
Tazama, jinsi ilivyo vyema, na kupendeza,
Ndugu kuishi pamoja, kwa umoja.
Kwa kuwa nawapa mafundisho mazuri;
Msiiache sheria yangu.
Mtu hulifurahia jibu la kinywa chake;
Na neno linenwalo wakati wa kufaa ni jema kama nini!
Mwanangu, ule asali, kwa maana ni njema,
Na sega la asali lililo tamu ulionjapo.
Basi utaijua hekima kuwa tamu kwa nafsi yako;
Ikiwa umekwisha kuiona;
Ndipo itakapofuata thawabu;
Wala tumaini lako halitabatilika.
Hekima ni njema kama urithi;
Naam, nayo ni bora kwao walionalo jua.
BWANA ni mwema kwa hao wamngojeao,
Kwa hiyo nafsi imtafutayo.
Ni vema mtu autarajie wokovu wa BWANA
Na kumngojea kwa utulivu.
Ee mwanadamu, yeye amekuonesha yaliyo mema; na BWANA anataka nini kwako, ila kutenda haki, na kupenda rehema, na kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako!
Basi torati ni takatifu, na ile amri ni takatifu, na ya haki, na njema.
Wala msifuate kanuni za dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.
Basi, huo wema wenu usitajwe kwa ubaya.
Basi, kabla ya mambo yote, nataka dua, na sala, na maombezi, na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote; kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, tuishi maisha ya utulivu na amani, katika utauwa wote na ustahivu. Hili ni zuri, nalo lakubalika mbele za Mungu Mwokozi wetu;
Kwa maana kila kiumbe cha Mungu ni kizuri, wala hakuna cha kukataliwa, kama kikipokewa kwa shukrani; kwa kuwa kimetakaswa kwa neno la Mungu na kwa kuomba.
Kila kutoa kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu, hushuka kwa Baba wa mianga; kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeukageuka.
Chumvi ni njema; lakini chumvi ikiwa si chumvi tena, mtaitia nini ikolee? Muwe na chumvi ndani yenu, mkakae kwa amani ninyi kwa ninyi.