Baraka za kuwa na umoja
Wimbo wa kupanda mlima.
1 Mwa 13:8;1 Kor 1:10 Tazama, jinsi ilivyo vyema, na kupendeza,
Ndugu kuishi pamoja, kwa umoja.
2 Kut 30:25 Ni kama mafuta mazuri kichwani,
Yashukayo ndevuni, ndevu za Haruni,
Yashukayo mpaka upindo wa mavazi yake.
3 Kum 4:48;28:8;Law 25:11;Dan 12:2,3;Mt 25:34,46;Yn 4:14;17:3;Ebr 7:25;1 Yoh 5:20 Ni kama umande wa Hermoni ushukao milimani pa Sayuni.
Maana huko ndiko BWANA alikoamuru baraka,
Naam, uzima hata milele.