1 Zab 34:11;Mit 1:8 Wanangu, yasikilizeni mausia ya baba yenu,
Tegeni masikio mpate kujua ufahamu.
2 Kwa kuwa nawapa mafundisho mazuri;
Msiiache sheria yangu.
3 2 Sam 12:24;1 Nya 29:1 Maana nilikuwa mwana kwa baba yangu,
Mpole, mpenzi wa pekee wa mama yangu.
4 1 Nya 28:9;Efe 6:4 Naye akanifundisha, akaniambia,
Moyo wako uyahifadhi maneno yangu;
Shika amri zangu ukaishi.
5 Jipatie hekima, jipatie ufahamu; usiusahau;
Wala usiyakatae maneno ya kinywa changu.
6 2 The 2:10 Usimwache, naye atakusitiri;
Umpende, naye atakulinda.
7 Mt 13:44;Lk 10:42 Bora hekima, basi jipatie hekima;
Naam, kwa mapato yako yote jipatie ufahamu.
8 1 Sam 2:30;Dan 12:3 Umtukuze, naye atakukuza;
Atakupatia heshima, ukimkumbatia.
9 Atakupa neema kuwa kilemba kichwani;
Na kukukirimia taji la uzuri.
10 Mwanangu, sikiliza, na kuzipokea kauli zangu;
Na miaka ya maisha yako itakuwa mingi.
11 Nimekufundisha katika njia ya hekima;
Nimekuongoza katika mapito ya unyofu.
12 Zab 18:36;91:11;Mit 3:23;4:19;Yer 13:16;Yn 11:9,10 Uendapo, hatua zako hazitadhiikika,
Wala ukipiga mbio hutajikwaa.
13 Mkamate sana elimu, usimwache aende zake;
Mshike, maana yeye ni uzima wako.
14 Usiingie katika njia ya waovu,
Wala usitembee katika njia ya wabaya.
15 Jiepushe nayo, usipite karibu nayo,
Igeukie mbali, ukaende zako.
16 Maana hawalali isipokuwa wametenda madhara;
Huondolewa usingizi, ikiwa hawakumwangusha mtu.
17 Maana wao hula mkate wa uovu,
Nao hunywa divai ya ujeuri.
18 Mt 5:14;Flp 2:15;2 Sam 23:4 Bali njia ya wenye haki ni kama nuru ing’aayo,
Ikizidi kung’aa hata mchana mkamilifu.
19 1 Sam 2:9;Ayu 5:14;Isa 59:9,10;Yer 13:16;Yn 12:35 Njia ya waovu ni kama giza;
Hawajui ni kitu gani kiwakwazacho.
20 Mwanangu, sikiliza maneno yangu;
Tega sikio lako, uzisikie kauli zangu.
21 Zisiondoke machoni pako;
Uzihifadhi ndani ya moyo wako.
22 Maana ni uhai kwa wale wazipatao,
Na afya ya mwili wao wote.
23 Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo;
Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.
24 Jiepushe na kinywa cha ujeuri,
Na midomo ya upotovu uiweke mbali nawe.
25 Macho yako yatazame mbele,
Na kope zako zitazame mbele yako sawasawa.
26 Ebr 12:13 Ulisawazishe pito la mguu wako,
Na njia zako zote zithibitike;
27 Isa 1:16 Usigeuke kwa kulia wala kwa kushoto;
Ondoa mguu wako maovuni.