Publicidade

Homem

Por Bíblia Online

A Bíblia fala sobre o homem como criação de Deus — feito à sua imagem e semelhança, mas também frágil, mortal e necessitado de redenção.

Criado à imagem de Deus

Deus criou o homem à sua imagem. Mas pelo pecado, o homem caiu e passou a depender da graça para ser restaurado.

Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila kiumbe kitambaacho nchini. Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.

Kisha wakasikia sauti ya BWANA Mungu, akitembea bustanini wakati wa jua kupunga; Adamu na mkewe wakajificha kati ya miti ya bustani, BWANA Mungu asiwaone.

Adamu na Kristo

Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi;

Ndivyo ilivyoandikwa, Mtu wa kwanza, Adamu, akawa kiumbe aliye hai; Adamu wa mwisho ni roho yenye kuhuisha. Lakini hautangulii ule wa roho, bali ule wa asili; baadaye huja ule wa roho. Mtu wa kwanza atoka katika nchi, ni wa udongo. Mtu wa pili atoka mbinguni. Kama alivyo yeye wa udongo, ndivyo walivyo walio wa udongo; na kama alivyo yeye wa mbinguni, ndivyo walivyo walio wa mbinguni. Na kama tulivyoichukua sura yake yule wa udongo, kadhalika tutaichukua sura yake yeye aliye wa mbinguni.

Fragilidade humana

O homem nascido de mulher é de poucos dias e cheio de inquietação. Deus conhece nossa fragilidade e cuida de nós.

Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke

Siku zake za kuishi si nyingi, naye hujaa taabu.

Je! Binadamu atakuwa na haki kuliko Mungu?

Je! Mtu atakuwa safi kuliko Muumba wake?

Je! Mtu ni kitu gani, hata ukamtukuza,

Na kumtia moyoni mwako,

Mwanadamu ni nini hata umkumbuke,

Ama mwana wa binadamu, hata umwangalie?

Mwenendo wa mtu watoka kwa BWANA;

Basi, awezaje mtu kuelewa na njia yake?

Renovação e chamado

Despojados do velho homem e revestidos do novo, somos chamados a buscar a justiça, a piedade e o amor.

mvue mwenendo wenu wa kwanza, utu wa zamani unaoharibika, kwa kuzifuata tamaa zenye kudanganya; na mfanywe wapya katika roho ya nia zenu; na mkavae utu mpya, ulioumbwa kwa namna ya Mungu katika haki na utakatifu wa kweli.

Naye akiisha kuuondoa ule uadui kwa mwili wake; ndiyo sheria ya amri zilizo katika maagizo; ili afanye hao wawili kuwa mtu mpya mmoja ndani ya nafsi yake; akafanya amani.

Vita vizuri vya imani

Bali wewe, mtu wa Mungu, uyakimbie mambo hayo; ukafuate haki, utauwa, imani, upendo, subira, upole.

Nilipokuwa mtoto mchanga, nilisema kama mtoto mchanga, nilifahamu kama mtoto mchanga, nilifikiri kama mtoto mchanga; tokea hapo nilipokuwa mtu mzima, nimeyabatilisha mambo ya kitoto.

Kwa maana njia za mwanadamu ziko mbele ya macho ya BWANA,

Na mienendo yake yote huitafakari.

Maandalio ya moyo ni ya mwanadamu;

Bali jawabu la ulimi hutoka kwa BWANA.

A confiança errada

Maldito o homem que confia no homem. O homem de duplo ânimo é instável em todos os seus caminhos.

BWANA asema hivi,

Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu,

Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake

Na moyoni mwake amemwacha BWANA.

Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana. Mtu wa nia mbili husitasita katika njia zake zote.

Huduma kwa waumini

Mzee usimkemee, bali umwonye kama baba; na wanaume vijana kama ndugu;

Seja o primeiro
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_19-25-13-