Honestidade
A honestidade é virtude cristã fundamental. Deus é Deus de verdade e nos chama a viver com integridade, transparência e retidão em todos os nossos relacionamentos e negócios.
Integridade diante de Deus
O Senhor abomina a balança falsa, mas o peso justo é seu prazer. A integridade dos justos os guia pelos caminhos retos.
Mizani ya udanganyifu ni chukizo kwa BWANA;
Bali vipimo vilivyo sawasawa humpendeza.
Ukamilifu wao wenye haki utawaongoza
Bali ukaidi wao wenye fitina utawaangamiza.
Ukamilifu wao wenye haki utawaongoza
Bali ukaidi wao wenye fitina utawaangamiza.
Ndipo utakapofahamu haki na hukumu,
Na adili, na kila njia njema.
Kutenda haki na hukumu
Humpendeza BWANA kuliko kutoa sadaka.
Macho yako yatazame mbele,
Na kope zako zitazame mbele yako sawasawa.
lakini tumekataa mambo ya aibu yaliyositirika, wala hatuenendi kwa hila, wala kulichanganya neno la Mungu na uongo; bali kwa kuidhihirisha iliyo kweli twajionesha kuwa na haki, dhamiri za watu zikitushuhudia mbele za Mungu.
tukitangulia kufikiri yaliyo mema, si mbele za Bwana tu, ila na mbele ya wanadamu.
Praticar a honestidade
Falai a verdade, pagai o que deveis, não negueis ao próximo o bem. A honestidade prática é testemunho do evangelho.
Msiambiane uongo, kwa kuwa mmevua kabisa utu wa kale, pamoja na matendo yake;
Wapeni wote haki zao; mtu wa kodi, kodi; mtu wa ushuru, ushuru; astahiliye hofu, hofu; astahiliye heshima, heshima.
Kwa sababu hiyo tena mnalipa kodi; kwa kuwa wao ni wahudumu wa Mungu, wakidumu katika kazi iyo hiyo.
Msimlipe mtu ovu kwa ovu. Angalieni yaliyo mema machoni pa watu wote.
Usiwanyime watu mema yaliyo haki yao,
Ikiwa katika uwezo wa mkono wako kuyatenda.
Afadhali mali kidogo pamoja na haki,
Kuliko mapato mengi pamoja na udhalimu.
Hazina za uovu hazifaidii kitu;
Bali haki huokoa na mauti.
Confissão e transparência
Confessai as vossas ofensas uns aos outros. Quem confessa e deixa o pecado encontra misericórdia e restauração.
Afichaye dhambi zake hatafanikiwa;
Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema.
Basi ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, ili mpate kuponywa. Sala yake mwenye haki ina nguvu nyingi, na hutenda mengi.
Lakini zaidi ya yote, ndugu zangu, msiape, wala kwa mbingu wala kwa nchi; wala kwa kiapo kinginecho chote; bali "ndiyo" yenu na iwe ndiyo, na "Hapana" yenu iwe hapana, msije mkaanguka katika hukumu.
Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina, haina unafiki.
Tukisema ya kwamba tunashirikiana naye, huku tukienenda katika giza, tunasema uongo, wala hatuifanyi iliyo kweli;
Watoto wadogo, tusipende kwa neno, wala kwa ulimi, bali kwa tendo na kweli.
Coração puro
Bem-aventurados os puros de coração, porque verão a Deus. A honestidade começa no interior e se manifesta nas ações.
Heri wenye moyo safi;
Maana hao watamwona Mungu.
Utulie mbele za BWANA,
Nawe umngojee kwa subira;
Usihangaike juu ya afanikiwaye katika njia yake,
Wala mtu apangaye maovu.
Heri atendaye fadhili na kukopesha;
Atengenezaye mambo yake kwa haki.
Jitahidi kujionesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mfanyakazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli.
Hakuna mtu ambaye akiisha washa taa huifunika kwa mtungi, au kuiweka mvunguni, bali huiweka juu ya kiango, ili waingiao wapate kuona nuru yake.
Katika kosa la midomo kuna mtego kwa mbaya;
Bali mwenye haki atatoka katika taabu.
Atamkaye maneno ya kweli hufunua haki;
Bali shahidi wa uongo hutamka hila.
Mtu mshupavu huleta fitina;
Na mchongezi huwafarakanisha rafiki.