1 Haleluya.
Heri mtu yule amchaye BWANA,
Apendezwaye sana na maagizo yake.
2 Wazawa wake watakuwa hodari duniani;
Kizazi cha wenye adili kitabarikiwa.
3 Mit 3:16;15:6;Isa 33:6;Mt 6:33;2 Kor 6:10 Nyumbani mwake mna utajiri na mali,
Na haki yake yadumu milele.
4 Nuru huwaangaza wenye adili gizani;
Ana fadhili na huruma na haki.
5 Lk 6:35 Heri atendaye fadhili na kukopesha;
Atengenezaye mambo yake kwa haki.
6 Kwa maana hataondoshwa kamwe;
Mwenye haki atakumbukwa milele.
7 Hataogopa habari mbaya;
Moyo wake u imara ukimtumainia BWANA.
8 Moyo wake umethibitika hataogopa,
Hata awaone watesi wake wameshindwa.
9 Lk 11:41;Rum 12:13;Mdo 4:35;20:35;2 Kor 8:9;9:9;1 Tim 6:18 Ametoa kwa ukarimu, na kuwapa maskini,
Haki yake yakaa milele,
Pembe yake itatukuzwa kwa utukufu.
10 Lk 13:28 Asiye haki ataona na kusikitika,
Atasaga meno yake na kuondoka,
Matumaini ya wasio haki hupotea.