Pular para o conteúdo
Publicidade

Justiça

Por Bíblia Online

A justiça é atributo de Deus e vocação do cristão. A Bíblia chama os crentes a buscar a justiça, praticar o que é reto e confiar no Deus que julga justamente.

Buscar a justiça

Buscai primeiro o Reino de Deus e a sua justiça. Quem semeia justiça colherá galardão seguro e duradouro.

Lakini utafuteni kwanza ufalme wa Mungu na haki yake, na haya yote atawapa pia.

Mtu mwovu hupata ujira wa udanganyifu,

bali yeye apandaye haki huvuna tuzo ya uhakika.

Yeye afuatiaye haki na upendo

hupata uzima, mafanikio na heshima.

Kufanya yaliyo sawa na haki inakubalika

zaidi kwa Mwenyezi Mungu kuliko dhabihu.

Njia zote za mwanadamu huonekana sawa kwake,

bali Mwenyezi Mungu huupima moyo.

Hazina zilizopatikana kwa njia mbaya hazifai,

lakini uadilifu huokoa kutoka mautini.

Justiça em Cristo

Deus tornou Cristo a nossa justiça. Pela fé somos declarados justos diante de Deus — não por obras, mas pela graça.

Kwa maana Mungu alimfanya yeye asiyekuwa na dhambi kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kufanywa haki ya Mungu kupitia kwake Al-Masihi.

Kwa maana neema ya Mungu ambayo inawaokoa wanadamu wote imefunuliwa. Nayo inatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia, ili tupate kuishi maisha ya kiasi, ya haki na ya utaua katika ulimwengu huu wa sasa,

Mambo mazuri ya imani

Lakini wewe, mtu wa Mungu, yakimbie mambo haya yote. Fuata haki, utauwa, imani, upendo, saburi na upole.

Hatimaye, ndugu zangu, mambo yote yaliyo ya kweli, yoyote yaliyo na sifa njema, yoyote yaliyo ya haki, yoyote yaliyo safi, yoyote ya kupendeza, yoyote yenye staha, ukiwepo uzuri wowote, pakiwepo chochote kinachostahili kusifiwa, tafakarini mambo hayo.

Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi. Kwa kuwa kile apandacho mtu ndicho atakachovuna.

Hivyo, tusichoke katika kutenda mema, kwa kuwa tutavuna kwa wakati wake tusipokata tamaa.

Praticar a justiça

O fruto da justiça semeia-se em paz para os que promovem a paz. Os olhos do Senhor estão sobre os justos.

Mavuno ya haki hupandwa katika amani na wale wafanyao amani.

Kwa hiyo, ungamianeni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana ili mpate kuponywa. Maombi ya mwenye haki yana nguvu, tena yanafaa sana.

Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia. Itakaseni mikono yenu ninyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu ninyi wenye nia mbili.

Kwa kuwa Mwenyezi Mungu huwapenda wenye haki

naye hatawaacha waaminifu wake.

Watalindwa milele,

lakini uzao wa waovu utakatiliwa mbali.

Macho ya Mwenyezi Mungu huwaelekea wenye haki,

na masikio yake yako makini kusikiliza kilio chao.

Hakika hatatikisika kamwe,

mtu mwenye haki atakumbukwa milele.

Furaha ya kweli

Heri mtu yule ambaye haendi

katika shauri la watu waovu,

wala hasimami katika njia ya wenye dhambi,

au kuketi katika baraza la wenye mizaha.

Ninakutafuta kwa moyo wangu wote,

usiniache niende mbali na amri zako.

Consequências

O Senhor recompensará cada um segundo suas obras. A justiça exalta a nação e traz segurança aos que a praticam.

Kwa maana Mungu atamlipa kila mtu kulingana na matendo yake.

Angalieni kuwa mtu asimlipe mwenzake maovu kwa maovu, bali siku zote tafuteni kutendeana mema ninyi kwa ninyi na kwa watu wote.

Lakini hata ikiwalazimu kuteseka kwa ajili ya haki, mmebarikiwa. "Msiogope vitisho vyao, wala msiwe na wasiwasi."

Tena mkiwatendea mema wale tu wanaowatendea ninyi mema, mwapata sifa gani? Hata wenye dhambi hufanya vivyo hivyo.

Ni mtego kwa mtu kuweka wakfu kitu kwa haraka

na baada ya kitambo kidogo kufikiria tena nadhiri zake.

Seja o primeiro

Este artigo te tocou? Faça uma oração!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.