8 Watu kutoka Sidoni na Arvadi walikuwa wapiga makasia yako;
watu wako wenye ustadi, ee Tiro,
walikuwa ndio mabaharia wako.
9 Wazee wa Gebali27:9 Yaani Bubilo, mji wa zamani sana wa Ufoinike (kama kilomita 80 kaskazini mwa Beiruti). pamoja na mafundi stadi
walikuwa mafundi wako melini.
Meli zote za baharini na mabaharia wao
walikuja kwako ili kubadilishana bidhaa zako.