8 Wakaaji wa Sidoni na Arvadi walikuwa wapiga makasia yako;
watu wako wenye ustadi, ee Tiro,
ndio walikuwa mabaharia wako.
9 Wazee wa Gebali27:9 yaani Bubilo pamoja na mafundi stadi
walikuwa mafundi wako kwenye meli.
Meli zote za baharini na mabaharia wao
walikuja kwako ili kubadilishana bidhaa zako.