Pular para o conteúdo
Publicidade

Isaya 54:9,10

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

9 "Kwangu mimi jambo hili ni kama siku za Noa,

nilipoapa kuwa maji ya Noa kamwe hayatafunika tena dunia.

Hivyo sasa nimeapa sitawakasirikia ninyi,

kamwe sitawakemea tena.

10 Ijapotikisika milima, na vilima viondolewe,

hata hivyo upendo wangu usiokoma kwenu hautatikisika,

wala agano langu la amani halitaondolewa,"

asema Bwana, mwenye huruma juu yenu.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    9 "Kwangu mimi jambo hili ni kama siku za Nuhu,

    nilipoapa kuwa maji ya Nuhu kamwe hayatafunika tena dunia.

    Hivyo sasa nimeapa sitawakasirikia ninyi,

    kamwe sitawakemea tena.

    10 Ijapotikisika milima, na vilima viondolewe,

    hata hivyo upendo wangu usiokoma kwenu hautatikisika,

    wala agano langu la amani halitaondolewa,"

    asema Mwenyezi Mungu, mwenye huruma juu yenu.

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    9 Yer 31:35;Mwa 9:8-17Kwa maana jambo hili limekuwa kama maji ya Nuhu kwangu; maana kama nilivyoapa ya kwamba maji ya Nuhu hayatapita juu ya dunia tena, kadhalika nimeapa ya kwamba sitakuonea hasira, wala kukukemea. 10 Zab 46:2;89:33Maana milima itaondoka, na vilima vitaondolewa; bali wema wangu hautaondoka kwako, wala agano langu la amani halitaondolewa; asema BWANA akurehemuye.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.