9 "Kwangu mimi jambo hili ni kama siku za Nuhu,
nilipoapa kuwa maji ya Nuhu kamwe hayatafunika tena dunia.
Hivyo sasa nimeapa sitawakasirikia ninyi,
kamwe sitawakemea tena.
10 Ijapotikisika milima, na vilima viondolewe,
hata hivyo upendo wangu usiokoma kwenu hautatikisika,
wala agano langu la amani halitaondolewa,"
asema Mwenyezi Mungu, mwenye huruma juu yenu.