Publicidade

Isaías 12

Kushukuru na kusifu

1 Katika siku ile utasema:

"Nitakusifu wewe, Ee Mwenyezi Mungu.

Ingawa ulinikasirikia,

hasira yako imegeukia mbali

nawe umenifariji.

2 Hakika Mungu ni wokovu wangu;

nitamtumaini wala sitaogopa.

Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu,

ni nguvu zangu na wimbo wangu;

amekuwa wokovu wangu."

3 Kwa furaha mtachota maji

kutoka visima vya wokovu.

4 Katika siku hiyo mtasema:

"Mshukuruni Mwenyezi Mungu, mliitie jina lake;

julisheni miongoni mwa mataifa yale aliyoyafanya,

tangazeni kuwa jina lake limetukuka.

5 Mwimbieni Mwenyezi Mungu, kwa kuwa ametenda mambo makuu,

hili na lijulikane duniani kote.

6 Pazeni sauti mwimbe kwa furaha, watu wa Sayuni,

kwa maana mkuu ni yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli miongoni mwenu."

Veja também

Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-16_18-40-07-