Publicidade

Atos 2

17 " Katika siku za mwisho, asema Mungu,

nitamimina Roho wangu

juu ya wote wenye mwili.

Wana wenu wa kiume na wa kike watatabiri,

vijana wenu wataona maono,

na wazee wenu wataota ndoto.

18 Hata juu ya watumishi wangu, wanaume kwa wanawake,

katika siku zile nitamimina Roho wangu,

nao watatabiri.

19 Nami nitaonesha maajabu juu mbinguni,

na ishara chini duniani:

damu, moto, na mawimbi ya moshi.

20 Jua litakuwa giza

na mwezi utakuwa mwekundu kama damu,

kabla ya kuja siku ile kuu ya Mwenyezi Mungu

iliyo tukufu.

21 Na kila mtu atakayeliitia

jina la Mwenyezi Mungu, ataokolewa.

Veja também

Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_19-25-13-